Inapakia video
Nakala
Swahili, Tanzania (Kiswahili)
Nimeona vema mimi nami kwa kuwa nimejitafutia usahihi wa mambo hayo yote tangu mwanzo
kukuandikia kwa taratibu Toefilo mtukufu ili upate kujua hakika ya mambo yale uliyofundishwa.
Siku zile Kaisari Agusto alipotawala Rumi na Herode mkuu akiwa mfalme wa Uyahudi,
malaika Gabrieli alitumwa na Mungu kwenda mpaka mji wa Nazareti kumtembelea bikira. Na bikira huyo aliitwa Mariamu.
Usiogope Mariamu kwa maana umepata neema toka kwa Mungu.
Tazama utachukua mimba, na kuzaa mtoto mwanamume na jina lake utamwita “Yesu”.
Itakuwaje?
Sijui mume.
Roho Mtakatifu atakujilia juu yako
kwa sababu hiyo, kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu, Ufalme wake hautakuwa na mwisho.
Mariamu akasafiri kwenda mji wa Yuda kumwamkia Binamu yake Elizabeti
ambaye pia alipokea muujiza wa ujauzito.
Elizabeti!
Mariamu!
Binamu Mariamu!
Umebarikiwa wewe katika wanawake,
naye uzao wa tumbo lako amebarikiwa.
Baada ya kusikia salamu zako,
mtoto aliye ndani yangu,
aliruka kwa furaha.
Moyo wangu wamwadhimisha Bwana,
na roho yangu inamfurahia Mungu mwokozi wangu.
Tokea sasa vizazi vyote wataniita mbarikiwa.
Sikieni enyi watu wa Nazareti; amri imetoka kwa Kaisari Augusto,
Kuhesabu orodha ya watu wa ulimwengu ikiwemo Galilaya na Yuda.
Basi imewapasa watu wote kuandikishwa katika miji na vijiji walikozaliwa.
Na Mariamu akaenda Bethlehemu ya Uyahudi Kujiandikisha. Pamoja na Yusufu mchumba wake.
Lakini hakukuwa na nafasi kwenye nyumba ya wageni.
Sehemu pekee walioweza kupata nafasi ni katika zizi la kulishia ngombe.
Na katika nchi ile ile walikuwako wachungaji wakikaa makondeni wakilisha kondoo wao wakati wa usiku.
Mara malaika wa Bwana akawatokea ghafla, utukufu wa Bwana ukawang'aria pande zote.
Leo katika mji wa Daudi amezaliwa Mwokozi Kristo Bwana.
Wachungaji wakaenda haraka kwenda kumwona mtoto aliyezaliwa katika zizi,
wakawa wa kwanza kuhubiri habari njema au injili ya mwokozi aliyezaliwa na mwanamke bikira.
Baada ya juma moja muda ulipofika wa mtoto kutahiriwa alipewa jina Yesu.