Inapakia video
Nakala
Swahili, Tanzania (Kiswahili)
Hakuna mtu aiwashaye taa na kuifunika kwa chombo.
Au huiweka uvunguni.
Bali huiweka juu ya kinara,
ili waingiao wapate kuona nuru yake.
Kwa maana hakuna neno lililositirika ambalo halitafunuliwa.
Wala lililofichwa ambalo halitajulikana na kuonekana wazi.
Jiangalieni msikiavyo,
kwa kuwa mwenye kitu atapewa,
Na yule asiye na kitu, atanyang'anywa hata ambacho anadhani anacho.
Mwalimu,
mama yako na ndugu zako wako nje,
wataka kukuona.
Mama na ndugu zangu ni walisikiao neno la Mungu
na kulitii.