This film is a perfect introduction to Jesus through the Gospel of Luke. Jesus constantly surprises and confounds people, from His miraculous birth to His rise from the grave. Follow His life through excerpts from the Book of Luke, all the miracles, the teachings, and the passion.
God creates everything and loves mankind. But mankind disobeys God. God and mankind are separated, but God loves mankind so much, He arranges redemption for mankind. He sends his Son Jesus to be a perfect sacrifice to make amends for us.
Before Jesus arrives, God prepares mankind. Prophets speak of the birth, the life, and the death of Jesus.
Jesus attracts attention. He teaches in parables no one really understands, gives sight to the blind, and helps those who no one sees as worth helping.
He scares the Jewish leaders, they see him as a threat. So they arrange, through Judas the traitor and their Roman oppressors, for the crucifixion of Jesus. They think the matter is settled. But the women who serve Jesus discover an empty tomb. The disciples panic. When Jesus appears, they doubt He's real. But it's what He proclaimed all along: He is their perfect sacrifice, their Savior, victor over death. He ascends to heaven, telling His followers to tell others about Him and His teachings.
Mungu ni mkuu sana. Uweza wake ni mkuu kuliko vyote.
Aliumba mbingu na nchi na vyote ndani yao.
Tukiangalia kila kitu Mungu alichofanya inashangaza.
Kila kitu Mungu alichoumba kilikuwa chema. Cha onyesha ukuu na wema na uweza wake.
Mungu aliumba mimea na wanyama.
Kisha, akamfanya mtu kutoka udongo.
Ali mpulizia puani pumzi yake, na kumpa uhai.
Mtu huyu wa kwanza aliitwa Adamu.
Kisha Mungu alichukua ubavu mmoja wa Adamu,
Na kutoka huo akamuumba mwanamke kuwa mke na mwenzi wake. Aliitwa Hawa.
Mungu aliumba mwanaume na mwanamke, na baadhi ya sifa zake,
ili waweze kufurahia uhusiano wa karibu naye.
Waliishi kwa furaha katika uwepo wake katika bustani nzuri iliyoitwa Edeni.
Mungu alimwambia Adamu;
Unaweza kula matunda yo yote ya miti katika bustani, kasoro mmoja.
Ikiwa utakula tunda kutoka mti huo utakufa.
Siku moja Shetani alimjaribu Hawa, kula tunda lile.
Alichukua lile tunda akala sehemu, na pia mumewe akala.
Walifanya hivi kwa sababu walimwamini Shetani kuliko Mungu. Hapo hapo uhusiano wao na Mungu ulivunjika.
Sababu Mungu ni mtakatifu, na wenye dhambi hawawezi kuishi alipo.
Hivyo Mungu alimfukuza Adamu na Hawa Kutoka bustani ya Edeni.
Waliteseka kwa aibu hii, kwa sababu hawakumtii Mungu.
Matokeo yake kwa Adamu na Hawa na uzao wao wote ni mateso na kifo.
Lakini Mungu ni wa rehema nyingi. Aliendelea kuwapenda sana wanadamu.
Alikuwa ameandaa njia kwa wao kurudi, Na kuishi katika ushirika naye tena.
Katika maandiko Mungu anaonyesha mpango wake wa kuokoa wanadamu,
kutoka adhabu waliyostahili, kwa kuondowa dhambi yao na aibu.
Mungu alionyesha sehemu ya mpango huu kwa Abrahamu.
Abrahamu alimtegemea Mungu na kumheshimu.
Mungu alimwahidi kumbariki na kubariki watu wa mataifa yote kupitia yeye.
Alimwahidi kumpa uzao mwingi kama mchanga wa bahari.
Na nyota za angani.
Abrahamu alimwamini Mungu, Mungu akamhesabia kuwa ni mwenye haki sababu ya imani hiyo.
Siku moja Mungu alimjaribu Abrahamu kuona kama angeweza kumtegemea na kutii amri zake.
Alimwambia kumchukua mtoto wake na kumtoa sadaka.
Abrahamu alijua kwamba ilikuwa kupitia mtoto huyo mmoja Mungu alimwahidi kumpa uzao mwingi.
Bado alimtegemea Mungu na kumtii.
Kwa hiyo alijiandaa kumwua mtoto wake, kuwa sadaka kwa Mungu.
Abrahamu aliinua kisu chake,
”Lakini Mungu alisema; usimdhuru mtoto. Najua kwamba una mcha Mungu, na uko tayari kunitii.
Kisha Abrahamu aliona kondoo karibu, amejishika pembe zake katika kichaka.
Abrahamu alimchukua kondoo, na kumtoa sadaka kwa Mungu badala ya mtoto wake.
Wakati Mungu alitoa kondoo kama sadaka, ili kufa badala ya mtoto wa Abrahamu.
Alimwonyesha upendo wake mkuu kwa watu.
Upendo wake ni kama upendo alio nao baba kwa mtoto wake.
Kupitia tukio hili, Mungu alionyesha kwamba alipanga kutoa sadaka, ili kufa badala ya wanadamu.
Hapo zamani Mungu alionyesha kwa manabii kwamba,
angemtuma mtu asiye na dhambi. Ili afe badala ya uzao wa Adamu. Na kuindoa dhambi na aibu yao.
Kwa sadaka yake kuu, angefungua njia kwa wale ambao wanamwamini,
na waishi katika ushirika na Mungu, katika Ufalme wa Mungu.
Manabii walimwita mtu huyu “Masihi”.
Walisema kwamba Mungu angemtuma Masihi, kuokoa watu na kuwatawala milele katika jina la Mungu.
Mamia ya miaka kabla hajaja,
manabii walisema kuhusu mambo ambayo Masihi angefanya, na mambo ambayo yangelimtokea.
Nabii Daudi alisema kwamba Mungu angemwelezea Masihi, “Wewe ni Mwanangu”.
Manabii walitumia jina la “Mwana wa Mungu” kuelezea uhusiano wa karibu na Mungu.
Na wajibu wake kama Mwokozi na Mfalme wa watu wote ulimwenguni.
Nabii Isaya alisema, “bikira atapata mimba na kuzaa mtoto”.
Mtoto wake ataitwa Emanueli, maana yake Mungu pamoja nasi.
Manabii waliandika kwamba Masihi angezaliwa Bethlehemu.
Na kwamba angeingia Yerusalemu kama Mfalme wao juu ya punda.
Pia waliandika kwamba, rafiki wakaribu angemsaliti kwa vipande thelathini vya fedha.
Manabii walisema kwamba, Masihi angetoa maisha yake. Lakini Mungu angemfufua kutoka kwa wafu.
Manabii pia walisema Masihi angekuja kama mwanadamu
katika mawingu na kwamba Mungu angempa mamlaka juu ya mataifa yote milele.
Miaka 2.000 iliyopita, mtu mmoja aliishi ulimwenguni, jina lake aliitwa Yesu.
Je! maisha ya Yesu, yalitimiza kile manabii walisema kuhusu “Masihi”?
Filamu hii yaonyesha Yesu ni nani. Na baadhi ya mambo aliyosema na kufanya. Kama alivyo andikwa katika maandiko.
Katika filamu hii, kuna mwigizaji wa nafasi ya Yesu. Hakuna mtu ye yote anayestahili kufanya hivi.
Lakini filamu hii imetengenezwa ili watu waweze kujua na kujifunza kuhusu maisha ya Yesu.
Na kupokea baraka ambazo Mungu ameahidi.
Nimeona vema mimi nami kwa kuwa nimejitafutia usahihi wa mambo hayo yote tangu mwanzo
kukuandikia kwa taratibu Toefilo mtukufu ili upate kujua hakika ya mambo yale uliyofundishwa.
Siku zile Kaisari Agusto alipotawala Rumi na Herode mkuu akiwa mfalme wa Uyahudi,
malaika Gabrieli alitumwa na Mungu kwenda mpaka mji wa Nazareti kumtembelea bikira. Na bikira huyo aliitwa Mariamu.
Usiogope Mariamu kwa maana umepata neema toka kwa Mungu.
Tazama utachukua mimba, na kuzaa mtoto mwanamume na jina lake utamwita “Yesu”.
Itakuwaje?
Sijui mume.
Roho Mtakatifu atakujilia juu yako
kwa sababu hiyo, kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu, Ufalme wake hautakuwa na mwisho.
Mariamu akasafiri kwenda mji wa Yuda kumwamkia Binamu yake Elizabeti
ambaye pia alipokea muujiza wa ujauzito.
Elizabeti!
Mariamu!
Binamu Mariamu!
Umebarikiwa wewe katika wanawake,
naye uzao wa tumbo lako amebarikiwa.
Baada ya kusikia salamu zako,
mtoto aliye ndani yangu,
aliruka kwa furaha.
Moyo wangu wamwadhimisha Bwana,
na roho yangu inamfurahia Mungu mwokozi wangu.
Tokea sasa vizazi vyote wataniita mbarikiwa.
Sikieni enyi watu wa Nazareti; amri imetoka kwa Kaisari Augusto,
Kuhesabu orodha ya watu wa ulimwengu ikiwemo Galilaya na Yuda.
Basi imewapasa watu wote kuandikishwa katika miji na vijiji walikozaliwa.
Na Mariamu akaenda Bethlehemu ya Uyahudi Kujiandikisha. Pamoja na Yusufu mchumba wake.
Lakini hakukuwa na nafasi kwenye nyumba ya wageni.
Sehemu pekee walioweza kupata nafasi ni katika zizi la kulishia ngombe.
Na katika nchi ile ile walikuwako wachungaji wakikaa makondeni wakilisha kondoo wao wakati wa usiku.
Mara malaika wa Bwana akawatokea ghafla, utukufu wa Bwana ukawang'aria pande zote.
Leo katika mji wa Daudi amezaliwa Mwokozi Kristo Bwana.
Wachungaji wakaenda haraka kwenda kumwona mtoto aliyezaliwa katika zizi,
wakawa wa kwanza kuhubiri habari njema au injili ya mwokozi aliyezaliwa na mwanamke bikira.
Baada ya juma moja muda ulipofika wa mtoto kutahiriwa alipewa jina Yesu.
Nao Yusufu na Mariamu wakamchukua mtoto na kumpeleka Yerusalemu kumweka wakfu kwa Bwana.
Ndani ya hekalu kulikuwepo na mtu mcha Mungu ambaye Roho Mtakatifu
alikuwa amemwahidi kuwa hatakufa mpaka amwone Kristo. Jina lake lilikuwa Simioni.
Sasa Bwana wamruhusu mtumishi wako aondoke kwa amani kama ulivyosema.
Kwa kuwa macho yangu yameuona wokovu wako.
Mtoto huyu amechaguliwa na Mungu.
Mungu awabariki nyote.
Baada ya miezi kadhaa, waliondoka wakarudi nyumbani kwao Nazareti.
Wakati Yesu alipofikisha miaka kumi na mbili,
Yusufu na Mariamu walimchukua mpaka Yerusalemu kwa ajili ya sherehe za pasaka.
Lakini walipokuwa wakirudi nyumbani wakifikiri kwamba mvulana alikuwa pamoja nao, Yesu alibaki nyuma.
Wakarudi mjini kumtafuta, na siku ya tatu wakamkuta Hekaluni ameketi pamoja na waalimu na wazee.
Ni mtoto wa nani aulizaye maswali ya jinsi hii?
Anatoka Nazareti.
Tulifikiri tumeondoka naye.
Tafadhali mruhusuni.
Wote waliomsikiliza walishangazwa.
Mwanangu, mbona umetutenda hivi? Baba yako na mimi tulikuwa tukikutafuta sana.
Kwa nini kunitafuta, hamkujua ya kuwa imenipasa kuwapo katika nyumba ya Baba yangu?
Na ikatokea akashuka pamoja nao mpaka Nazareti, Naye akizidi kukua akiongezeka katika hekima na kimo.
Akimpendeza Mungu na wanadamu.
Katika mwaka wa kumi na tano wa kutawala kwake Kaisari Tiberio,
Pontio Pilato alipokuwa liwali wa Uyahudi,
Na Herode mfalme wa Galilaya,
na Anasi na Kayafa makuhani wakuu.
Neno la Bwana likamjia Yohana Mbatizaji jangwani
Na akafika inchi yote akihubiri ubatizo wa toba iletayo ondoleo la dhambi.
Ziacheni dhambi zenu,
mkabatizwe,
Mungu atawasamehe dhambi zenu.
Kama ilivyo andikwa katika kitabu cha nabii Isaya:
Sauti ya mtu aliaye nyikani:
tengenezeni njia ya Bwana!
Yanyosheni mapito yake.
Kila bonde litajazwa;
na kila mlima na kilima kushushwa!
Palipopotoka patakuwa pamenyooka, na palipo kwaruza pata lainishwa.
Na wote wenye mwili
watauona wokovu wa Mungu.
Tufanye je? Naam tuambie tufanyeje?
Enyi kizazi cha nyoka!
Wataka tufanyeje?
Tuambie. Tugeukie njia ipi?
Aliye na kanzu
mbili
ampe mtu yule
asiye
nayo.
Na mwenye chakula
vivyo hivyo.
Mwalimu!
Tuu watoza ushuru,
tufanyeje?
Msitoze zaidi ya mlivyoamriwa!
Na sisi je?
Yatupasaje?
Msimdhulumu kitu mtu ye yote.
Msimshtaki mtu kwa uwongo.
Toshekeni na mishahara yenu.
Tuambie…
wewe ndiwe Kristo?
Nawabatiza kwa maji.
lakini yuaja mtu mwenye nguvu kuliko mimi.
Mimi sistahili hata kulegeza kamba za viatu vyake. Yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.
Pepeto lake li, mkononi mwake. Naye atausafisha sana uwanda wake, na kuikusanya ngano ghalani mwake.
Na Roho Mtakatifu akashuka juu ya Yesu kwa mfano wa kiwiliwili kama hua.
Na sauti ikatoka mbinguni ikisema: “Wewe ndiwe Mwanangu mpendwa wangu nimependezwa nawe.”
Yesu alipoanza kazi yake alikuwa Amepata umri wa miaka thelathini.
Akarudi kutoka Yordan akiwa amejaa Roho Mtakatifu.
Na akaongozwa na Roho jangwani aliko jaribiwa na Shetani kwa mda kwa siku arobaini.
Katika mda wote huu hakula chochote.
Kisha Shetani akamwambia:
“Ikiwa ndiwe mwana wa Mungu, liamuru jiwe hili liwe mkate!”
Imeandikwa
kwamba mtu hataishi kwa mkate tu, bali kwa neno la Mungu.
Kisha Shetani akampandisha juu kumwonyesha milki zote za ulimwengu.
Nitakupa wewe enzi hii yote na fahari yake
kwa kuwa imo mikononi mwangu. Nami humpa ye yote kama nipendavyo.
Basi wewe ukinisujudia yote yatakuwa yako.
Imeandikwa msujudie Bwana Mungu wako,
Umwabudu yeye peke yake”.
Kisha Shetani akamwongoza mpaka Yerusalemu akamweka juu ya kinara cha hekalu.
Ikiwa wewe ndiye mwana wa Mungu jitupe chini,
Maana imeandikwa: “atakuagizia malaika zake Wakulinde"
“Kwamba usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.”
Imeandikwa,
“usimjaribu Bwana Mungu wako.”
Na akaenda Nazareti hapo alipolelewa.
Habari?
Nzuri!
Na siku ya sabato akaingia katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake.
Akasimama ili asome, akapewa kitabu cha nabii Isaya.
Roho wa Bwana yu juu yangu.
Amenituma kuwahubiri maskini habari njema.
Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, na vipofu kupata kuona.
Kuwaacha huru waliosetwa,
na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubalika kuwaokoa watu wake.
Anena vema!
Leo maandiko haya yametimia
masikioni mwenu.
Yametimia!,
Ni Masihi pekee awezaye kutimiza ahadi hii.
Tutajuaje?
Hapana shaka mtaniambia methali hii,
Tabibu jiponye!
Mtaniambia kwamba,
yaliyotendeka Kapernaumu
Yatende na hapa kwenu.
nawaambia kwamba,
hakuna nabii akubalikaye kwao.
Kwa maneno haya Yesu alijitambulisha kama Masihi, mpakwa mafuta wa Mungu, aliyetumwa kuwaokoa watu wake.
Wayahudi hawakumkubali kama Masihi.
Wakataka kumtupa ukingoni mwa kilima.
Lakini yeye akapita katikati ya umati
na kwenda zake.
Hadi Kapernaumu mji wa Galilaya.
Utawala wa Kirumi ulionekana waziwazi kila mahali.
Watu wakamtazamia Masihi kwa shauku ili awakomboe kutoka katika uonevu waliokuwa wakiupata.
Amani iwe kwenu!
Nawe Bwana!
Simoni chombo chako chaweza kunibeba?
Kwa nini isiwe!
Anataka kuondoka, siyo?
Sema nasi! Sema nasi!
Sema nasi!
Yesu, sema nasi!
Palikuwapo na watu wawili waliopanda kwenda hekaluni kusali.
Mmoja farisayo na wa pili mtoza ushuru.
Farisayo akasimama akaomba hivi moyoni:
“E! Mungu, nakushukuru kwa kuwa mimi si kama watu wengine.
Wanyang'anyi, wadhalimu, wazinzi, wala huyu mtoza ushuru”.
Nafunga mara mbili kwa juma,
hutoa zaka katika mapato yangu yote.
Lakini yule mtoza ushuru alisimama mbali, wala hakuthubutu hata kuinua macho yake mbinguni,
alijipiga kifua akisema,
“E! Mungu niwie radhi mimi mwenye dhambi”.
Nawaambia mtoza ushuru alishuka kwenda nyumbani kwake amehesabiwa haki kuliko yule.
Kila mtu ajikwezaye, atadhiriwa.
Naye ajidhiriye
atakwezwa.
Twekeni chombo chenu mpaka kilindini.
Kisha mshushe nyavu zenu mvue samaki.
E, Bwana,
tumehangaika usiku kucha.
Hatukupata kitu.
Lakini kwa neno lako,
nitashusha nyavu.
Yakobo!
Yohana!
Haha! Haha! Haha! Haha!
Yakobo! Yohana! Leteneni chombo.
Upesi tumeelemewa.
Yatosha! Yatosha!
Haha! haha haha!
Ondoka kwangu Bwana,
mimi ni mwenye dhambi.
Usiogope,
sasa utakuwa mvuvi wa watu.
Tegeni masikio yenu na kunijia, sikieni na nafsi zenu zitaishi.
Mtafuteni Bwana, maadamu anapatikana. Mwiteni maadamu yu karibu.
Mtu mbaya na aache njia yake,
na mtu asiye haki aache mawazo yake, na amrudie Bwana, naye atamrehemu.
Na arejee kwa Mungu wetu, naye atamsamehe kabisa.
Maana mtatoka kwa furaha na mtaoongozwa kwa amani.
Anakuja, yuko hapa.
Yesu!
Yesu!
Ninakusihi ukamponye binti yangu!
Nihurumiye,
ana miaka kumi na miwili tu,
yu katika kufa, naomba tafadhali, njoo nami!
Yairo! Pole sana!
Yesu,
Binti yako amesha kufa,
Usinisumbue mwalimu.
Usiogope,
amini tu naye ataponywa.
Msilie,
hajafa bali amelala tu.
Mtoto,
amka!
Mpeni kitu cha kula.
Nawaambia,
msimwambie mtu yoyote kilichotokea.
Na baadaye akamwona mtoza ushuru aitwaye Mathayo ameketi forodhani akipokea kodi.
Nifuate!
Na Yesu aliondoka akaenda mlimani ili kuomba. Akakesha usiku kucha katika kumwomba Mungu.
Na kulipokuwa mchana aliwaita wanafunzi wake, akawachagua kumi na wawili,
miongoni mwao ambao aliwaita mitume.
Simioni aliyemwita Petro,
na Andrea ndugu yake,
Yakobo,
na Yohana,
Filipo,
na Batholomeo,
na Mathayo,
na Tomaso,
na Yakobo mwana wa Alfayo,
na Simoni aitwaye Zelote,
na Yuda ndugu yake na Yakobo,
na Yuda Iskariote aliyemsaliti.
Heri mlio maskini,
ufalme wa Mungu ni wenu.
Heri mlio na njaa sasa kwa sababu mtashiba.
Heri mliao sasa kwa sababu mtacheka.
Heri watu watakapo wachukia na kuwatenga,
Na kuwashutumu kwa ajili ya Mwana wa Adamu.
Furahini yatakapotokea na kurukaruka.
Tazama thawabu yenu ni kubwa mbinguni.
Baba zao waliwatenda manabii vivyo hivyo.
Kumi na sita, kumi na saba, kumi na nane, Kumi na tisa, ishirini.
Hicho ndicho nilicho nacho kwa sasa.
Una maana gani ndicho tu, ulicho nacho?
Ole wenu mlio na mali,
faraja yenu mmekwisha kuipata.
Ee, hehehe! ee, hehehe! Ee, hehe!
Hataki utajiri atakuwa na matatizo kweli,
Ole wenu ninyi mnao cheka sasa,
kwa kuwa mtaomboleza na kulia.
Ole wenu ninyi watakapo wasifu,
kwa kuwa baba zao waliwatenda manabii wa uongo mambo kama hayo.
Lakini nawaambia ninyi mnaonisikia,
wapendeni adui zenu,
watendeeni mema wanao wachukia,
wabarikini wanao walaani,
waombeeni wa watendeao maovu.
Akupigaye shavu moja,
mgeuzie na la pili.
Akunyang'anyae joho lako, usimzuilie na kanzu.
Mpe kila akuombaye.
Akunyang'anyae vitu vyako,
usitake akurudishie.
Watendeeni,
yale tu mnaotaka watu wawatendee.
Mkiwapenda tu wale wano wapenda ninyi,
Mwaonyesha fadhili gani?
Kwa kuwa hata wenye dhambi, huwapenda wale wanaowapenda.
Mkiwatendea mema wale wawatendeao mema,
Mwaonyesha fadhili gani?
Hata wenye dhambi hufanya hivyo.
Anamgusaje?
Awezaje kuongea naye?
Yachukiza!
La!
Wapendeni adui zenu.
Na watendeeni mema.
Mkopeshapo msitamaini kurudishiwa.
Na thawabu yenu itakuwa nyingi.
Kwa kuwa mtakuwa wana wa Mungu aliye juu.
Kwa maana yeye ni mwema kwa wasiyo Mshukuru na waovu.
Iweni na huruma,
kama Baba yenu alivyo na huruma.
Yesu tuokoe!
Msihukumu nanyi hamtahukumiwa.
Msilaumu,
nanyi hamtalaumiwa.
Sameheni,
nanyi mtasamehewa.
Tuongoze, eee, Bwana!
Toeni nanyi pia mtapewa.
Kwakuwa kipimo kile mpimacho ndicho mtacho pimiwa.
Kipofu hawezi kumwongoza kipofu mwenzie.
Akifanya hivyo wote wawili watatumbukia shimoni.
Kwa nini watazama kibanzi kwenye jicho la ndugu yako, na wewe huoni boriti kwenye jicho lako?
Tuongoze ee, Bwana!
Twakuhitaji ee, Bwana!
Heri mwanamke aliye kuzaa na ku kunyonyesha.
Hahaha!
Wana heri wale walisikiao neno la Mungu,
na kulishika.
Napenda kumjua mtu huyu.
Je wafikiri aweza kuwa
ni Masihi?
Farisayo huyu alimwalika Yesu ale chakula pamoja naye nyumbani kwake. Yesu akaketi ili apate kula.
Sikilizeni watoto ondokeni,
mmenisikia?
Nenda?
Wanakwenda kwa ujeuri wao, lakini ni watoto wazuri.
Anafanya nini hapa?
Sijui!
Anafanya nini hapa?
Mtu huyu angekuwa nabii angemtambua, mwanamke huyu anaye mgusa.
Angejua jinsi anavyoishi maisha ya dhambi.
Simoni, ninamjua mwanamke huyu.
Ngoja nikwambie kitu;
Mtu mmoja mkopeshaji alikuwa na wadeni wawili.
Mmoja alimdai denari 500, na wa pili 50.
Na walipokuwa hawana cha kumlipa,
aliwasamehe wote wawili.
Ni yupi atakaye mpenda zaidi?
Ni yule ambaye amesamehewa nyingi.
Umeamua haki.
Wamwona mwanamke huyu,
nili ingia nyumbani kwako hukunipa maji kwa ajili ya miguu yangu.
Bali huyu amenidondoshea machozi miguu yangu. Na kuipangusa kwa nywele zake.
Wewe hukunibusu,
lakini huyu tangu nilipoingia hakuacha kunibusu miguu yangu.
Hukunipaka kichwa changu mafuta,
Lakini huyu amenipaka miguu yangu marhamu.
Basi nakwambia,
dhambi zake nyingi amesamehewa, kwa kuwa amependa sana.
Lakini aliyesamehewa kidogo,
hupenda kidogo.
Umesamehewa dhambi zako.
Anawezaje kusema hivi? Awezaje kusamehe dhambi? Anakufuru!
Imani yako imekuokoa nenda kwa amani.
Na Yesu alikuwa akizunguka zunguka, akihubiri na kutangaza habari njema za Ufalme wa Mungu.
Na wale mitume kumi na wawili waliambatana naye pamoja.
Na Baadhi ya wanawake aliowaponya na magonjwa mabaya na mapepo.
Mariamu aitwaye Magdalene,
Yoana mke wa Kuza wakili wa Herode.
Na Suzana.
Lakini Herode mtawala wa Galilaya, aliyewekwa na Warumi, alimfunga Yohana Mbatizaji gerezani,
kwa kuwa alimshutumu kwa kumchukua mke wa nduguye.
Amesema je?
Tulipofika kwenye lango la Naini,
tulikutana na msafara wa msiba.
Huyu marehemu alikuwa mtoto wa pekee wa mwanamke mjane.
Yesu alipomwona alijaa huruma akagusa jeneza na kusema,
“kijana nakuamuru inuka.”
Kisha ile maiti ikainuka, na Yesu akamkabidhi kwa mamaye.
Mwulizeni,
semeni,
wewe ndiye yule ajaye aliyesema Yohana?
au tumtarajie mwingine?
Bwana!
Bwana!
Yohana Mbatizaji ametutuma tukuulize
ikiwa wewe ndiye yule ajaye,
au tumtazamie mwingine?
Nendeni mkamweleze Yohana mlioyaona na kuyasikia.
Vipofu wanaona,
na viwete wanatembea.
Heri mtu yule asiyekuwa na shaka nami.
Naomba unibebe.
Unaweza kuona sasa ukiwa begani kwangu?
Namwona Yesu sasa.
Mpanzi alitoka kwenda kupanda mbegu zake.
Alipokuwa akipanda nyingine zikaanguka karibu na njia, zi kanyagwa
na ndege wa angani wakazila.
Zingine zikaanguka kwenye mwamba.
Zilipoanza kumea, zikakauka kwa kukosa rutuba.
nyingine zikaanguka katika miiba,
na miiba ikamea pamoja nazo,
ikazisonga.
Nyingine zikaanguka kwenye udongo mzuri,
na zile mbegu zikakua,
zikazaa moja kwa 100.
Bwana,
kwanini unaongea kwa mifano kila kukiwa na kusanyiko?
Ninyi mmepewa kuzijua siri za ufalme wa Mungu.
Bali wengine kwa mifano, ili wakiona, wasione,
Wakisikia, wasielewe.
Maana yake ni hii:
Mbegu ni neno la Mungu.
Wale wa karibu na njia, ndiyo wasikiao,
kisha ibilisi akaliondoa hilo neno mioyoni mwao wasije wakaamini hilo neno na kuokoka.
Walio kwenye mwamba ndio wale wasikiapo na hulipokea lile neno kwa furaha,
bali hawana mizizi.
Huamini kwa kitambo kidogo,
wakati wa kujaribiwa,
hujitenga.
Zilizoanguka kwenye miiba ni waliosikia,
Na katika kuenenda kwao husongwa na shughuli, na mali, na anasa za maisha haya
wasiivishe lolote.
Na zilizo anguka kwenye udongo mzuri,
ni ambao kwa unyoofu wa wema wa mioyo yao, hulisikia neno na kulishika.
Kisha huzaa matunda kwa kuvumilia.
Hakuna mtu aiwashaye taa na kuifunika kwa chombo.
Au huiweka uvunguni.
Bali huiweka juu ya kinara,
ili waingiao wapate kuona nuru yake.
Kwa maana hakuna neno lililositirika ambalo halitafunuliwa.
Wala lililofichwa ambalo halitajulikana na kuonekana wazi.
Jiangalieni msikiavyo,
kwa kuwa mwenye kitu atapewa,
Na yule asiye na kitu, atanyang'anywa hata ambacho anadhani anacho.
Mwalimu,
mama yako na ndugu zako wako nje,
wataka kukuona.
Mama na ndugu zangu ni walisikiao neno la Mungu
na kulitii.
Ikawa siku zile, Yesu akapanda chomboni na wanafunzi wake. Aka waambia na tuvuke mpaka ng'ambo ya ziwa.
Nao walipokuwa wakienda alilala usingizi.
Bwana!
Bwana!
Yesu!
Tunaangamia!
Mawimbi yanatukabili karibu tuna zama. Tuokoe Bwana Mkubwa!
Tutaokoka!
Imani yenu iko wapi?
Wakafika pwani ya nchi ya Wagerasi inayoelekea Galilaya.
Ehhh,ehhh,harrriii…
Ehhh,ehhh,harrriii…
Yesu!
Mwana wa Mungu aliye juu,
Nina nini nawe?
Nakuomba,
usinitese!
Jina lako nani?
Jeshi!
Bwana tunakusihi!
Usi...
usitutupe shimoni!
Tuache tuingie
kwa wale
nguruwe.
Ehhh!
Haya rudini!
Simama!
Simama!
Pepo wakamtoka mtu yule,
Rudini!
wakaingia kwa nguruwe.
Ondoka mahali hapa!
Mchawi wewe!
Tuache, ondoka mahali hapa tuache!
Tuache!
Ondoka mahali hapa!
Nitakufuata popote uendako!
Niruhusu
nikafuate!
Rudi nyumbani,
ukahubiri Mungu aliyokutendea.
Yesu akawachukua wanafunzi wake akaenda nao faraghani Bethsaida.
Na makutano walipojua, walimfuata.
Baadaye jioni, Petro akasema:
Bwana,
waage makutano
ili waende vijijini na mashambani, karibu na hapa,
wapate chakula na pa kulala. Tulipo, ni nyika tupu.
Wapeni ninyi chakula!
Hatuna! ila mikate mitano na samaki wawili.
Ubarikiwe Eeee! Bwana Mungu wetu, Mfalme wa ulimwengu, utupae chakula hapa duniani.
Ni muujiza!
Siamini!
Watu husema mimi ni nani?
Wengine wanasema, wewe ni Yohana Mbatizaji.
Wengine husema wewe ni Eliya.
Na wengine wanasema mmoja wa manabii wa kale
amefufuka.
Nanyi mnasemaje?
Mimi ni nani?
Ndiwe Kristo wa Mungu.
Msimwambie mtu ye yote neno hili:
Inampasa Mwana wa Adamu kupata mateso mengi.
Na kukataliwa,
na kuuwawa na siku ya tatu kufufuka.
Je? Kuna yeyote atakaye nifuata?
Nitakufuata Bwana Mkubwa.
Lakini kwanza,
nipe ruhusa
nikawaage watu wa nyumbani kwangu.
Mtu aliyetia mkono wake kwa kulima, kisha akaangalia nyuma, hafai kwa ufalme wa Mungu.
Mtu yeyote akitaka kunifuata na ajikane mwenyewe,
ajitwike msalaba wake na anifuate.
Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake ataiangamiza,
na mtu atakayeingamiza nafsi yake kwa ajili yangu ndiye atakayeisalimisha.
Yamfaa nini mtu kuupata ulimwengu wote na kisha kupoteza nafsi yake?
Mtu akinionea haya mafundisho yangu,
Mwana wa adamu naye atamuonea haya atakapo kuja katika utukufu.
Utukufu wa Baba na malaika wake.
Nawaambia kweli,
baadhi ya walio hapa hawataonja mauti, hata waone kwanza ufalme wa Mungu.
Kisha Yesu akawatoa Yohana na Yakobo, na Petro, Akaenda nao kuomba mlimani.
Naye alipokuwa akisali sura ya uso wake ikageuka. Mavazi yake yakawa meupe.
Na tazama watu wawili wakawa wakizungumza naye. Nao ni Musa na Eliya walionekana katika utukufu.
Uta kamilisha kusudi la Mungu.
Uta fia Yerusalemu.
Walipokuwa wakiondoka, Petro akamwambia Yesu;
Bwana, ni vizuri sisi kuwepo hapa.
Na tujenge vibanda vitatu.
Kimoja chako,
Na Petro alipokuwa akiongea, wingu likawafunika nao wakaogopa sana.
kimoja cha Musa,
na kimoja cha Eliya.
Na sauti ikatoka katika wingu Huyu ni Mwanangu Mteule wangu msikieni yeye.
Mwalimu!
Mwalimu!
Nakuomba umwangalie mwanangu.
Tafadhali, tafadhali msaidie,
Yeye ni mwanangu wa pekee.
Nimewasihi wanafunzi wako wa mwombeye,
Lakini hawakuweza.
Enyi kizazi kisicho na imani, kilichopotoka,
Nitakaa na kuchukuliana nanyi hata lini?
Mlete mwanao hapa!
Uso wake umepona pia,
Ni ajabu!
Tufundishe kusali,
kama Yohana alivyowafundisha wanafunzi wake.
Msalipo semeni hivi:
“Baba yetu uliye mbinguni,
Jina lako litukuzwe,
Ufalme wako uje,
mapenzi yako yatimizwe hapa duniani kama huko mbinguni,
Utupe siku kwa siku riziki yetu,
Utusamehe dhambi zetu,
kwa kuwa sisi nasi tunawasamehe wote walio tukosea,
Usitutie majaribuni,
bali utuokoe nayule mwovu.”
Ombeni nanyi mtapewa,
Tafuteni nanyi mtaona,
Bisheni nanyi mtafunguliwa.
Kwa maana kila aombaye hupokea,
Na kila atafutaye huona,
Naye abishaye atafunguliwa.
Ha! ha! ha! ha! ha!
Ni yupi kwenu aliye baba, mwanaye kimwomba mkate atampa jiwe?
Au nyoka, badala ya samaki?
Au akiomba yai atampa nge?
Basi ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema,
Je? Baba yenu wa mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao wamwombao?
Nawaambia,
kwa sababu hiyo msisumbukie maisha yenu, mtakula nini,
au mtavaa nini,
Kwa kuwa maisha yenu ni zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya nguo.
Angalieni ndege wa angani,
Hawapandi, wala hawavuni, wala hawana ghala ya kutunzia chakula.
Lakini Mungu wenu huwalisha.
Je! Ninyi si wa thamani zaidi ya ndege?
Ni yupi kwenu ambaye akijisumbua, aweza kujiongezea kimo chake?
Ikiwa hamwezi hata jambo ndogo,
Kwa nini kujisumbua kwa ajili ya mengine?
Ya tafakarini maua,
jinsi yanavyomea,
Hayatendi kazi wala hayasokoti,
Hata Sulemani katika fahari yake yote, hakuvikwa vizuri kama hayo.
Ikiwa Mungu
huyavika hivi majani ya kondeni, yaliyoko leo na kesho hutupwa kalibuni,
Je? hatawatendeya ninyi zaidi?
Enyi wenye imani haba?
Tuongezee imani,
Kama mngekuwa na imani ndogo kama punje ya haradali,
mngeuambia mkuyu huu,
Ngoka na ukapandwe baharini, nao unge watii.
Makwazo hayana budi kuja,
Lakini ole wake ayasababishae.
Ingemfaa zaidi mtu huyo jiwe la kusagia lifungwa shingoni mwake, akatupwe baharini.
Kuliko kumkosesha mmoja wa wadogo hawa.
Ufalme wa Mungu unafanana na nini?
Unafanana na hivi:
Mtu anachukua punje ya haradali na kupanda shambani mwake.
Naye hukua na kuwa mti mkubwa.
Na ndege wa angani wakajenga viota juu yake.
Sina hakika anaongelea nini;
Mbona mnakula na kunywa pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi?
Wenye afya hawana haja ya tabibu,
Isipokuwa wagonjwa.
Sikuja kuwaita wenye haki kutubu,
bali wenye dhambi.
Twambie tena kuhusu Ufalme wa mbinguni,
Je? una kingine zaidi?
Msiogope enyi kundi ndogo, kwa kuwa Baba ameona vema kuwapa ufalme.
Uzeni vitu vyote mlivyo navyo mwape maskini.
Jifanyieni mifuko isiyochakaa, akiba isiyopungua, katika mbingu.
Mahali pasipo karibia wezi,
wala nondo kuharibu.
Hazina yenu ilipo ndipo itakapokuwa na mioyo yenu.
Mwanamke,
umepona ugonjwa wako.
Tazama, tazama, amepona! Ni muujiza, tazama amepona! Njooni mwone!
Bwa-Bwa-Bwa-Bwa-Bwana!
Asifiwe!
Miaka kumi na nane,
Mungu akubariki Mwalimu!
Twapaswa kufanya kazi siku sita,
njoo siku yo yote kati ya hizo na uponye.
Lakini siyo siku ya sabato.
Enyi wanafiki,
je? hamwatoi ng'ombe au punda kula majani? Au hamu wapi maji siku ya sabato?
Huyu mwanamke aliye uzao wake Ibrahimu, ambaye shetani amemfunga kwa miaka kumi na minane.
Je, hakupaswa afunguliwe siku ya sabato?
Mwalimu mwema nifanye nini nipate kurithi uzima wa milele?
Kwa nini waniita mwema?
Hakuna aliye mwema ila Mungu pekee.
Wazijua amri:
Usizini,
usiue, usimshuhudie jirani yako uwongo,
Waheshimu baba yako na mama yako,
haya yote nimeshika tangu utoto wangu.
Bado umepungukiwa na neno moja,
Viuze vyote ulivyo navyo wagawie maskini,
Na utakuwa na hazina mbinguni.
Kisha uje unifuate.
Lakini sisi tu wafanya biashara; matajiri.
Ni vigumu kweli kwa matajiri kuingia ufalme wa Mungu.
Ni vyepesi kwa ngamia kupita katika tundu la sindano,
Kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu.
Nani basi awezaye kuokoka?
Lisilowezekana kwa mwanadamu kwa Mungu lawezekana.
Ufalme wa Mungu.
Utakuja lini?
Ufalme wa Mungu hauji kwa kuuchunguza.
Wala hawatasema,
tazama huu hapa, na ule pale.
Kwa maana Ufalme wa Mungu umo ndani yenu.
Siku zinakuja mtakapo tamani kuona moja kati ya siku za Mwana wa adamu.
Msiione
Maana kama vile umeme umulika vyo toka upande huu, chini ya mbingu,
ndivyo atakavyokuwa siku ya Mwana wa Adamu katika siku yake.
Lakini kwanza ni lazima ateseke sana na akataliwe na watu wa kizazi hiki.
Ni rahisi kwa mbingu na nchi kupita kuliko hata nukta moja ya maandiko kutanguka.
Kwa hakika nawaambia kwamba manabii wengi na wafalme walitamani kuona mnayo ninyi, na hawakuweza.
Na kusikia mnayoyasikia ninyi, hawakuweza.
Tufanyeje?
Maandiko yasemaje?
na mnatafsiri vipi?
Mpende Bwana Mungu wako,
kwa moyo wako wote,
kwa roho yako yote,
kwa nguvu zako zote,
na kwa akili yako yote,
na mpende jirani yako kama nafsi yako.
Umejibu vema,
fanya hivyo nawe utaishi.
Jirani yangu ni nani?
Siyo wale askari,
wasemaje kuhusu Kaisari?
Mtu mmoja alisafiri kutoka Yerusalemu kwenda Yeriko.
Wanyang'anyi wakamshambulia.
Wakampiga, wakamvua nguo zake, na kumwacha karibu kufa.
Ikatokea kuhani alipopita njia ile, alipomwona akapita kando, na akaendelea na safari yake.
Na vivyo hivyo mlawi naye akapita pale, akamtazama kisha akaendelea na safari yake.
Lakini Msamaria mmoja aliyekuwa anasafiri njia ile, akamwona mtu yule,
alipomwona moyo wake ukajaa na huruma.
Akamwendea na kumpaka mafuta na divai na kuvifunika vyake na kuvifunika kwa vitambaa safi.
Kisha akampandisha kwenye mnyama wake, na kumpeleka kwenye nyumba ya kutunzia wageni, akamuuguza,
siku ya pili, akamlipa mwenye nyumba dinari mbili.
Na kumtaka aendelee kumtunza mtu yule.
Ni yupi kati ya watatu hawa aliyetenda kama jirani kwake mtu yule aliyeshambuliwa na wanyang'anyi?
Ni yule aliyemhurumia.
Ha ha ha! Ninyi pia fanyeni vivyo hivyo.
Waacheni watoto wadogo waje kwangu wala msiwazuie,
kwa maana ufalme wa Mungu ni wao.
Amini nawaambia,
ye yote asiyeupokea ufalme wa Mungu kama watoto hawa, hakika hatauingia.
Atakaye mpokea mmoja wa watoto hawa kwa jina langu, anipokea mimi.
Anipokeaye mimi, ampokea yule aliyenituma.
Aliye mdogo kwenu ninyi, ndiye aliye mkubwa.
Eeeeh! kuna nini, nini kinaendelea?
Ni Yesu wa Nazareti anapita.
Yesu!
Yesu!
Mwana wa Daudi! Nirehemu!
Wataka nikufanyie nini?
Bwana nipate kuona.
Upate kuona!
Imani yako imekuponya.
Naona!
Naona!
Naonaaaa!
He,he,he,heee!
Yesu alipokuwa anapanda kwenda Yerusalemu, mkutano mkubwa ulimfuata.
Watu walimwuliza awaonyesha njia ya wokovu. Na kuwafundisha zaidi kuhusu Ufalme wa Mungu.
Hakika mtu huyu ni nabii.
Bwana wangu niokoe!
Eeee! Bwana, tuokoe!, tuokoe!
Bwana asifiwe!
Bwana tuonyeshe njia ya kweli!
Watu walianza kumkubali kama Bwana. Na pale Yeriko, palikuwa na mtoza ushuru jina lake Zakayo.
Alitaka sana kumwona Yesu hata akapanda juu ya mti ili aweze kumwona.
Huyo ni mtoza ushuru!
Zakayo shuka chini,
kwa maana imenipasa kushinda nyumbani kwako leo.
Nyumbani kwangu!
Ni nani angetaka kukaa nyumbani kwake?
Zakayo amemjuaje Yesu?
Sikilizeni,
nitatoa
nusu ya mali yangu
kwa maskini.
Na kama
nimemdanganya mtu,
nitamrudishia
mara nne zaidi.
Siamini mtoza ushuru kurudisha kodi alizoiba!...Haiwezekani!
Wokovu umeingia nyumbani humu leo.
Kwa maana mtu huyu pia ni mwana wa Ibrahimu.
Mwana wa Adamu alikuja kutafuta kilichopotea.
Sikilizeni;
tunakwenda Yerusalemu.
Kila liloandikwa na manabii kwa Mwana wa Adamu litatimia.
Atatolewa kwa mataifa,
watamdhihaki,
na kumdharau, na kumtemea mate.
Atapigwa viboko na kuuawa.
Lakini siku ya tatu,
atafufuka tena.
Pamoja na kwamba Yesu alijua anakwenda kuuawa kwa dhambi za wanadamu, alishika njia kwenda Yerusalemu.
Watu wengi walifurahia ujio wake.
Na wakamtangaza Mfalme wao.
Mwalimu, waamuru wafuasi wako wanyamaze kimya.
Ninawaambia hawa, wakinyamaza,
Mawe yatapiga kelele.
Amani juu mbinguni na utukufu kwake Yeye aliye juu.
Yesu akakaribia Yerusalemu, alipouona mji, aliulilia machozi.
Laiti kama,
siku ya leo, ungejua njia ya amani, lakini umeshindwa kuiona.
Siku zinakuja maadui wako,
watajenga ngome na kukuzunguka na kubana kutoka pande zote.
Na katika kuta zoko watakuharibu,
wewe na watoto wako.
Na hawatasaza jiwe juu ya lingine. Kwa sababu hukuijua siku ya kujiliwa kwako.
Hekalu takatifu katika Yerusalemu, lilikuwa limekua kituo cha biashara, kuliko mahali pa ibada
Tano, sita, saba, nane, tisa, kumi,
kumi na moja, Kumi na mbili, kumi na tatu, kumi na nne, kumi na tano, kumi na sita,....
Imeandikwa,
nyumba yangu itakuwa nyumba ya sala.
Lakini ninyi mmeifanya pango la wanyang'anyi.
Anawafuatia wanyama wangu,
Mzuieni!
Mzuieni!
Waiteni walinzi! Waiteni walinzi!
Upinzani ukaongezeka miongoni mwa baadhi ya viongozi wa dini
na wa kisiasa kwa sababu watu walimtangaza Yesu kuwa ni Mfalme.
Nafahamu kwamba wengi wamemtambua kama yeye ni mfalme.
Mfalme!
Mfalme wa maskini wa makahaba na wezi.
Tumeona watu kama yeye kabla.
Wanakuja, wanatoa madai yao wanaondoka.
Na wamesahaulika.
Usiwe kipofu!
Wafuasi wake wanaongezeka kila siku.
Watu wanampenda.
Na anafikiri ni mfalme.
Ngoja ni wape onyo.
Ikiwa mtu huyu, atatishia amani zaidi,
nitawalaumu ninyi.
Labda yuko sahihi,
ni muda mwafaka wa kupambana naye.
kadri alivyozidi kuwashambulie waandishi na mafarisayo kwa unafiki wao,
ndivyo umaarufu wake miongoni mwa Wayahudi uliongezeka.
Na vivyo hivyo upinzani kutoka kwa wale waliompinga.
Yesu akiwa hekaluni, akamwona mama mjane, maskini akitoa senti mbili katika sadaka.
Huwezi kutowa zaidi?
Nawaambieni
huyu mama mjane maskini ametoa vingi kuliko wote.
Kwa maana wengine wametoa katika mabaki ya walivyo navyo.
Lakini yeye ametoa kutoka katika umaskini wake vyote alivyo navyo.
Tuambie,
kwa mamlaka ya nani unatenda haya?
Na nani aliye kupa mamlaka hii?
Nami nitauliza swali:
Niambieni, mamlaka ya ubatizo Yohana aliyapata kwa Mungu au kwa mwanadamu?
Tuseme nini?
Tukisema yatoka kwa Mungu,
atatuuliza mbona
hamkumwamini Yohana?
Lakini tukisema kwa wanadamu, watu wote hawa watatupiga mawe.
Wote waliamini kuwa Yohana alikuwa nabii.
Hatujui yalitoka wapi.
Hata mimi siwaambii kwa mamlaka ya nani nafanya haya yote.
Kulikuwa na mtu aliyelima shamba la mizabibu.
Akaajiri wafanyakazi.
Kisha akasafiri kwenda nchi ya mbali kwa muda mrefu.
Muda wa mavuno ulipofika,
akamtuma mtumwa wake kwa wale wafanya kazi,
kupokea sehemu yake ya mavuno.
Lakini wafanya kazi wakampiga na kumrudisha mikono mitupu.
Akamtuma mwingine.
Lakini wafanya kazi wakampiga na yeye pia, na kumtendea hiana, kisha wakamrudisha bila kitu.
Kisha akamtuma mtumwa wa tatu. Lakini wafanyakazi wakamjeruhi na kumtupa nje
Kisha mwenye shamba akajisemea; nifanye nini? Nitamtuma mwanangu mpenzi.
Hakika watamheshimu.
Lakini wale wafanyakazi, walipomwona wakaambiana:
Huyu ndiye mrithi.
Tumuue, kisha mali hii itakuwa ya kwetu.
Tuambie zaidi Bwana.
Hivyo wakamtupa nje ya shamba,
wakamuuwa.
Yule mwenye shamba atafanya nini na hao wakulima?
Atakuja na kuua wafanyakazi wote na kuwapa shamba wafanyakazi wengine.
Maandiko haya yana maana gani?
Jiwe walilolikataa waashi,
limekuwa jiwe kuu la pembeni.
Kila aangukaye juu yake, huvunjika, vunjika.
Na kila jiwe limwangukiae,
litamsaga kabisa.
Mwalimu,
tunajua kwamba wasema na kufundisha yaliyo ya haki.
Wala hujali cheo cha mtu awaye yote.
Bali hufundisha njia ya Mungu.
Tuambie,
Je, ni halali kwetu kumlipa Kaisari kodi, au siyo?
Jihadhari Bwana, anajaribu kutega!
Nionyesheni sarafu.
Ni sura na chapa ya nani iliyo kwenye sarafu hii?
Kaisari!
Mpeni Kaisari
yaliyo ya Kaisari,
na Mungu
yaliyo ya Mungu.
Jibu lako ni nini katika hilo?
Ikawa majira ya siku kuu ya mikate isiyotiwa chachu yaani pasaka, ilikaribia.
Yesu akamtuma Simoni Petro na Yohana, kutangulia mbele kumwaandalia chakula cha pasaka.
Nimetamani sana kuila pasaka hii pamoja nanyi kabla ya mateso yangu.
Nawaambia,
sitakula tena hata itakapotimizwa katika ufalme wa Mungu.
Ubarikiwe, Eee Bwana Mungu wetu,
Mfalme wa mbingu na nchi.
Utupae matunda katika mzabibu.
Twaeni hii mnywe miongoni mwenu.
Nawaambia sitakunywa tena katika matunda ya mzabibu, hata Ufalme wa Mungu utakapokuja.
Ubarikiwe, Eee Bwana Mungu wetu,
Mfalme wa mbingu na nchi.
Uletae mkate kutoka katika nchi.
Huu ni mwili wangu utolewao kwa ajili yenu.
Fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.
Hiki ni kikombe cha agano ya damu yangu, imwagikayo kwa ajili yenu.
Lakini tazameni mkono wake yule atakaye nisaliti uko pamoja nami hapa mezani.
Amini nawaambia Mwana wa Adamu atakwenda kama ilivyokusudiwa. Lakini ole wake mtu yule atakaye msaliti.
Haiwezekani!
Waniitaje msaliti!
Aliye mkuu kati yenu na awe mdogo kabisa.
Na kiongozi awe kama mtumwa.
Kwa maana nani ni mkuu?
Yeye aketiye chini kula?
Au yeye ahudumiae?
Ni yeye aketiye chini bila shaka.
Lakini mimi niko miongoni mwenu kama ahudumiae.
Mmekaa na mimi katika majaribu yangu yote.
Na kama Baba yangu alivyonipa haki ya kutawala,
Nami nawapeni haki hiyo hiyo.
Mtakula na kunywa katika meza yangu katika Ufalme wangu.
Na mtakaa katika kiti cha enzi kuhukumu makabila kumi na mbili ya Israel.
Basi hakuna msaliti!
Simoni, Simoni, tazama!
Shetani amewaka ninyi
apate kuwapepeta kama ngano. Akijaribu imani yenu.
Lakini nimekuombea Simoni kwamba imani yako isitindike.
Na ukisha kurudi kwangu, waimarishe ndugu zako.
Bwana,
niko tayari kwenda nawe kifungoni.
Na hata kufa pamoja nawe.
Nakwambia Petro,
jogoo hatawika leo, kabla wewe, hujanikana mara tatu.
Nilipo watuma bila mkoba, wala viatu, mlipungukiwa na jambo lolote?
Hapana,
hatukupungukiwa kitu.
Lakini sasa ye yote, mwenye mfuko auchukue.
Na asiye kuwa na upanga, auze vazi lake na kununuwa.
Nawaambia,
imeandikwa katika maandiko, alihesabiwa pamoja na wahalifu.
Kwa sababu yanipasayo, yana mwisho wake.
Tazama,
kuna panga mbili, Bwana!
Yatosha.
Na baraza La wazee walikakutana, kujadili namna gani kumwondoa Yesu.
Shetani akamwingia Yuda aliyeitwa Iskariote. Aliyekuwa miongoni mwa kumi na wawili.
Akala njama na wazee ili kumsaliti Yesu.
Yesu akatoka Yerusalemu akaenda mlima wa mizeituni kuomba.
Ombeni msije mkaingia majaribuni.
Yuda Iskariote alimsaliti Yesu kwa vipande thelathini vya fedha.
Yesu akijua saa ya kifo chake kwa ajili ya dhambi za wanadamu imekaribia akaomba;
Baba,
ikiwa ni mapenzi yako,
niondolee kikombe hiki.
Siyo kama nitakavyo mimi,
bali mapenzi yako yatimizwe.
Na malaika kutoka mbinguni, akamtokea akamtia nguvu.
Na jasho lililo mvuja, likawa kama matona ya damu, yakidondoka chini.
Kwa nini mnalala?
Amkeni,
na muombe msije mkaingia majaribuni.
Yuda!
Wamsaliti Mwana wa Adamu kwa kumbusu?
Bwana, je! tu wapige kwa upanga?
Haya mkamateni.
Yatosha!
Muujiza!
Mmenijia kwa mapanga na marungu kama mimi ni mhalifu,
Nilikuwa nanyi kila siku hekaluni na wala hamkunikamata.
Lakini hii ni saa yenu kutenda kazi.
Wakati nguvu za giza zinatawala.
Mkamateni!
Mlindeni vizuri!
Askari walimchukua mpaka kwenye ua, wakamdhihaki kwamba ni Mfalme wa wayahudi.
Hahahaha! Hii hapa kanzu inavaliwa na Mfalme!
Hahahaha! Twambie nini kinakwenda kutokea!
Hahahaha! Je!Utatuokoa?
Mtu huyu pia alikuwa na Yesu!
Mwanamke, simjuwi mtu huyu!
Niliwaona pamoja!
Tu, watumishi wako waaminifu, ha,ha,ha,haaaa!
Unajisikiaje ukimtazama?
Wewe pia ni mmoja wao.
Lakini si mimi.
Hapana shaka mtu huyu alikuwa na Yesu,
Kwa sababu yeye piya ni mgalilaya.
Nenda zako,
sijui ni nini unacho ongelea!
Yesu akageuka na kumwangalia Petro akamkazia macho.
Kisha Petro akakumbuka maneno ambayo Bwana alimwambia:
“Kabla jogoo haja wika hivi leo, utanikana mara tatu.”
Oooo! Bwana,
Tunakusihi,
fanya upendavyo,
kulingana na ukuu Wa nguvu zako.
Ohooo! Wewe,
uliyewasamehe baba zetu, walipo asi kinyume na neno lako.
Wewe,
japo uliwakasirikia,
lakini hukuwaangamiza.
Kwa sababu ya upendo wako kwao, na kwa ajili ya agano lako.
Wewe uliwarehemu.
Nani kakupiga, tabiri!
nani atakupiga tena!
Acheni!
Acheni nasema!
Mleteni mbele ya baraza.
Nenda!
Baraza la wazee na wakuu wa dini, walikutana kumjadili Yesu.
Tuambie,
wewe ndiye Masihi?
Hata nikiwaambia,
hamtaniamini.
Na nikiwauliza swali, hamtanijibu.
Lakini kuanzia sasa Mwana wa Adamu ataketi mkono wa kuume wa Mungu mwenyezi.
Tuambie,
ndiwe Mwana wa Mungu?
Wewe wasema Mimi ndiye.
Ni nani amekupa mamlaka ya kusema hivi?
Ana hatia!
Sisi wenyewe tumesikia yale aliyoyasema;
Tuta mpeleka kwa Pilato.
Mpelekeeni kwa Pilato yeye mwenyewe!
Tembea!
Wakampeleka mbele ya Pontio Pilato, liwali aliyekuwa katili kuliko watawala wote wakirumi.
Ambaye alikuwa amesulubisha maelfu.
Mnataka nini hapa? Hapa asubuhi namna hii?
Tulimkuta akipotosha taifa letu.
Ame sababisha ghasia katika mnada pale hekaluni.
Je! tumpe adhabu gani?
Auawe!
Sioni sababu yo yote kumhukumu mtu huyu. Sioni!
Tumeona anayo hatia.
Anawaambia watu wasilipe kodi kwa Kaisari.
Anadai kuwa yeye ndiye Kristo,
Mfalme!
Mfalme?
Wewe ni Mfalme wa Wayahudi?
Wewe wasema!
Alianzia kule Galilaya, na sasa amefika huku.
Galilaya?
Je! mtu huyu ni Mgalilaya?
Ikiwa hivyo,
Herode ashughulike naye.
Bado yuko Yerusalemu. Au sivyo.
Mpelekeni kwa Herode.
Wewe unasema kuwa u nani?
Na hao wafuasi wako ni akina nani?
Wengi wanasema waweza kufanya miujiza,
Nifanyie mmoja nione.
Bwana wangu,
amekuwa akiwaharibu watu wetu wote.
Eti anajiita,
Mfalme.
Mtu huyu?
Mfalme!, hahahahaha!
Mtukufu!
Mchape viboko barabara.
Mrudisheni kwa Pilato,
hili ndilo jimbo lake.
Mtu huyu
hajafanya chochote kinachostahili kufa.
Kwa hiyo apigwe mijeledi,
kisha tutamwachilia huru.
Ni lazima afunguliwe mtu mmoja wakati huu wa siku kuu.
Tufungulie,
Baraba!
Baraba. Ndiyo.
Mwondoshe mtu huyu.
Ndiyo, tufungulie Baraba.
Msulubishe!
Ndiyo, msulubishe!
Wewe wewe,
mpige mijeledi.
Una gojea nini Pilato?
Yeye ni Yesu!
Kwa nini mmemtesa hivyo.
Mwache yeye ni Kristo.
Haja fanya neno lo lote.
Mwinueni!
Lakini wakaendelea kupiga kelele kwa sauti kubwa kuwa Yesu asulubiwe.
Kwa hiyo Pilato, akamhukumu Yesu kifo, akamwacha huru Baraba.
Yule waliyemtaka, aliyekuwa amefungwa kwa kuua, na kusababisa ghasia. Akam kabidhi Yesu kwao asulubiwe.
Nyuma!
Rudi nyuma!
nyuma!
ondoka!
kaa mbali naye.
Rudi nyuma!
rudi nyuma!
nyuma!
Acha nafasi!
kaa mbali!
Toa njia,
Wee! Toka njiani.
Tembea imara nyooka kamili.
Inuka!
Inuka!
Wewe,
jina lako nani?
Simoni Mkerene mheshimiwa!
Karibia hapa!
Kata kamba!
Wewe beba!
Haya tembea!
Nyuma!
Nyuma!
achia njia!
Songa mbele! Achia njia hapo!
Nyuma!
Rudi nyuma!
Rudi nyuma!
Tuna kulilia Bwana, tunalia. Kunywa hayo, kunywa.
Kunywa Bwana.
Enyi binti za Yerusalemu,
Msinililie mimi.
Bali jililieni nafsi zenu na watoto wenu.
Kwa kuwa kama wametenda mambo haya kwa mti mbichi,
Itakuwaje kwa mti mkavu?
Mungu akusaidie.
Oooh! Tutakuombea!
Tembea,
Pita huku,
Haya!
Haraka,
Haraka,
Haya wee! Tembea,
Haraka! fanya hima, haraka
Sasa tembea
Tembea
Wee, tembea!
Kwenda sasa!
Endelea kupigilia
Inua msalaba!
Wewe pigilia mambo.
Legeza kamba.
Baba uwasamehe,
Kwa kuwa hawajui watendalo.
Aliokoa wengine,
na ajiokoe mwenyewe.
Ndiyo jiokoe mwenyewe ikiwa ndiwe Kristo. Shuka msalabani,
tuonyeshe mojawapo ya miujiza yako.
Na Yesu akasulubiwa kati ya wezi wawili,
ili kutimiza unabii kama nabii wa Mungu alivyotabiri, miaka mingi kabla.
Hii ni nguo ya ajabu, isiyo ya kawaida. Ahaaa! ahahahaaa!
Haya achia, hapana, usichane, nitawaambia.
Ebu na tulipigie kura.
Turushe sarafu, atakayepata kichwa ndiye mshindi.
Mi' nitakuwa wa kwanza.
Mi' ntakuwa wa pili.
Nipe sarafu. Nataka mimi nianze.
amerusha kichwa, nimeshinda! We, una bahati
Wewe kila siku unashinda.
Wakaweka kibao juu ya kichwa chake, kilicho andikwa, huyu ndiye Mfalme wa wayahudi.
Ikiwa wewe ni Mfalme wa Wayahudi jiokoe mwenyewe!
Je, wewe siye Kristo,
Jiokoe...
mwenyewe...
na sisi.
Wewe humwogopi Mungu?
Sote tumehukumiwa kusulubiwa.
Wewe umekosa,
yeye hana kosa lolote.
Yesu nikumbuke,
utakapokuja kama Mfalme.
Amini na kuambia,
leo hii utakuwa pamoja nami
peponi.
Hapo ilikuwa yapata saa sita. Kukawa na giza juu ya nchi yote hadi saa kenda. Juwa limepungua nuru yake.
Pazia la hekalu likapasuka toka juu hadi chini.
Baba,
mikononi mwako,
naiweka
roho yangu.
Yule akida alipoona yaliyotokea, alimtukuza Mungu akisema;
Utukufu kwa Mungu. Hakika huyu alikuwa mwenye haki.
Yusufu wa Arimathaya mmoja wasiyo baraza la dini, mtu mwenye haki, ambaye hakukubaliana na kitendo hiki,
akaenda kwa Pontio Pilato Kutaka apewe mwili wa Yesu. Akauchukue na kuuzika kaburini, kabla ya sabato haijaingia.
Tafadhali tunaufuata mwili wa Bwana wetu.
Wote mnakaribishwa.
Lakini njooni, sabato inakaribia.
Hata siku ya kwanza ya juma, alfajiri, walikwenda kaburini na manukato waliyo yaandaa.
Wakalikuta jiwe limeviringishwa mbali na kaburi. Lakini walipoingia kaburini, mwili wa Bwana Yesu haukuwepo.
Kwa nini mnamtafuta aliye hai kati ya wafu? hayupo hapa amefufuka.
Kumbukeni alivyowaambia, alipokuwa Galilaya;
Imempasa Mwana wa Adamu kutiwa mikononi mwa wenye dhambi. Na kusulubiwa, na kufufuka siku ya tatu.
Sikiliza,
jiwe limeviringishwa,
tukaingia ndani,
na mwili wa Bwana wetu
haukuwapo.
Mwili wa Bwana wetu haupo?
Watu wawili walitutoke,
malaika wanaong'aa
kama jua.
Wakatwaambia,
Kwanini mnamtafuta aliye hai
katika wafu?
Ni kweli,
tuaminini,
tuaminini.
Tuliwaona, nendeni mkaone. Kaburi li wazi, Bwana wetu hayupo.
Petro lazima utuamini.
Yesu akawatokea wawili kati ya wanafunzi, nao wakarudi kwa wengine kwa furaha.
Hakika Bwana amefufuka.
Amemtokea Simoni.
Hatukumtambuwa, kabisa
akiwa njiani,
alipomega mkate tu tukamtambua.
Huko Emaus, amewezaje kwenda huko, ajabu!
Amani iwe kwenu.
Mbona mnafadhaika?
Kwanini mnaona shaka mioyoni mwenu?
Tazama
mikono yangu na miguu yangu.
Muone kuwa ni mimi mwenyewe.
Nishikeni muone nanyi mtajua.
Kwa kuwa roho haina mwili na mifupa kama mnavyoniona mimi.
Haya ndiyo maneno niliyowaambia nilipokuwa nanyi.
Kwamba ni lazima yote niliyoandikiwa katika torati ya Musa, manabii na zaburi yatimizwe.
Hivyo ilivyoandikwa:
kwamba Kristo atateswa,
na kufufuka siku ya tatu.
Kwa jina lake
mataifa yote yatahubiriwa injili ya toba na ondoleo la dhambi.
Kuanzia tangu Yerusalemu.
Na ninyi ndiyo mashahidi wa haya.
Na tazama nawaletea juu yenu ahadi ya Baba yangu.
Lakini kaeni mjini humu kwanza,
hata mvikwe uweza utokao juu.
Bwana awabariki, awatunze.
Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.
Basi enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi,
na kuwabatiza kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu.
Na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi.
Na tazama mimi nipo pamoja nanyi siku zote hata ukamilifu wa dahari. Amen!
Zamani manabii waliandika katika maandiko, Kwamba Mungu angemtuma Masihi
kuokoa wenye dhambi na kuwapatanisha naye.
Maisha ya Yesu, yanaonyesha wazi,
kwamba hakika huyu Ndiye Mwokozi, ambaye Mungu aliahidi kumtuma ulimwenguni.
Nabii Isaya aliandika, bikira atachukua mimba na kuzaa mtoto mwanaume. Na hivyo ikatokea.
Mungu kwa uweza wake alisababisha Maria angali bado bikira kupata mimba na kuzaa mtoto Yesu.
Imeandikwa katika maandiko,
muujiza wa kuzaliwa kwake, Ilikuwa ni ishara ya Mungu kwamba, mtoto huyu alikuwa Ni Masihi,
ambaye Mungu alimwita Mwanaye.
Watu walipomwona Yesu, waliona asili na uweza wa Mungu.
Aliponya watu na kuwasamehe dhambi zao. Na kuwaahidi mahali katika Ufalme wake.
Yesu alitoa maisha yake, na kupata mateso Kwa ajili ya watu wote.
Kisha, alifufuka akionyesha kwamba uwezo wake ni mkubwa kuliko uwezo wa mauti.
Yesu Masihi alisema: Nina uwezo wa kuutoa uhai wangu, na uwezo wa Kuutwaa tena.
Maisha ya Yesu yalikuwa kama manabii walivyo andika kawmba, Masihi angekuwa.
Kweli, Yesu ni Neno la Mungu. Katika Yesu Mungu anajionyesha mwenyewe kwa watu wa ulimwengu huu.
Yesu Masihi alisema: Mbingu na dunia vitapita lakini maneno yangu hayatapita kamwe.
Hapo mwanzo Mungu alimumba mwanaume na mwanamke ili kwamba wangeishi na furaha kwake.
Lakini hawakumwamini Mungu na kutii amri zake. Kitendo hiki cha aibu kiliwatenganisha wao na Mungu.
Katika maandiko imeandikwa; Wote wamefanya dhambi, na mshahara wa dhambi ni mauti.
Watu waliofanya dhambi hawawezi kuishi katika uhusiano pamoja na Mungu.
Kama Mungu alivyo mtowa kondoo kufa badala ya mtoto wa Abrahamu,
Ndivyo Mungu alimtuma Yesu ili afe badala ya uzao wa Adamu.
Alifanya hivi ili wale wote ambao wanamwamini, nakuweka imani yao katika Bwana Yesu.
Waweze kwenda katika uwepo wake.
Petro alisema; Yesu ni yule ambaye manabii walitabiri.
Wakisema kwamba Mungu atasamehe dhambi za kila mtu atakaye mwamini.
Kwa hiyo, wale wamfuatao Yesu, wataepuka hukumu na wataishi na Mungu milele.
Wakati Yesu amefufuka kutoka wafu, alisema kwa wamfuatao: Watu watatangaza katika jina langu kwa mataifa yote,
Kwamba Mungu anasamehe dhambi, kwa wale wanaomgeukia Na kutubu.
Yesu alisema pia: Angetuma Roho Mtakatifu kwa wanafunzi wake ili kuwaonyesha kweli
na kuwapa uwezo wa kufuata njia ya Mungu.
Wakati mwanamke mwenye dhambi alipotubu dhambi zake Na kuanza kumfuata, Yesu alisema kwake:
Umesamehewa dhambi zako. Umeokolewa kwa sababu umeniamini.
Yesu alisema; watu wanapompenda Mungu kweli, Ni ushahidi kwamba Mungu amewasamehe dhambi zao.
Yesu Masihi aliwaita watu wamfuate.
Wakati mhalifu pale msalabani alimwamini Yesu Na kuomba kuokolewa, Yesu alisema:
Leo hii utakuwa nami peponi.
Wale ambao wanaamua kumfuata Yesu, Wanaweza kuanza uhusiano wao naye kwa Kutumia sala kama hii;
Mungu Baba, wewe ni mwenye haki. Nakushukuru kwamba unanipenda.
Najuta kwamba nimetenda dhambi, na kutotii amri zako.
Nashukuru kwamba ulimtuma Yesu kufa, Msalabani kwa niaba yangu. Na kwamba akafufuka toka kwa wafu.
Nakushukuru kwamba aliumia kwa adhabu Ya dhambi nilizozifanya.
Ninakupokea Yesu kama Bwana na Mwokozi wangu.
Nakushukuru kwamba umenisamehe dhambi zangu.
Na umefungua njia kwa ajili yangu, kuwa nawe daima.
Nakuomba unipe Roho Mtakatifu wako, awe nami Na kunionyesha njia yako.
Anipe uwezo ili nikupende wewe kwa moyo wangu wote. Na kuisha maishi yanayokupendeza.
Na watu waweze kukusifu wewe popote Ulimwenguni. Amen!
Yesu alisema kuhusu wamfuatao; Kondoo wangu waisikia sauti yangu, nami Nawajua, nao wanifuata.
Wamufuatao Yesu hukutana pamoja, Wanazungumza naye kila siku. Wanajifunza neno lake katika maandiko.
Wanatafuta kufuata mfano wake. Na wanawaambie wengine kuhusu Yeye.
Yesu huwasaidia wao na kuwatia nguvu kupitia uwezo wa Roho wa Mungu, ambaye anaishi ndani ya mioyo yao.
Wanaweka mioyoni mwao, yale Yesu aliyoyasema, Wakati akipanda juu kwenye kiti chake cha enzi mbinguni.
Mungu amenipa mamlaka yote mbinguni na duniani.
Kuwa na hakika na hili, nami nipo pamoja Nanyi daima hata mwisho wa ulimwengu.