Sehemu
Invitation to Know Jesus Personally
dakika 6FHD
Love Your Neighbor·5 kati ya 5Klipu 5 kati ya 5
Invitation to Know Jesus Personally
A narrator gives an invitation to know God personally. The invitation is open to everyone. It means turning to God and trusting Jesus with our lives and to forgive our sins. We can speak to Him in prayer when we're ready to become followers of Jesus.
MaswaliMaswali Yanayohusiana
Uliza lakoNukuu za Biblia
ShirikiNakala
Swahili, Tanzania (Kiswahili)
Zamani manabii waliandika katika maandiko, Kwamba Mungu angemtuma Masihi
kuokoa wenye dhambi na kuwapatanisha naye.
Maisha ya Yesu, yanaonyesha wazi,
kwamba hakika huyu Ndiye Mwokozi, ambaye Mungu aliahidi kumtuma ulimwenguni.
Nabii Isaya aliandika, bikira atachukua mimba na kuzaa mtoto mwanaume. Na hivyo ikatokea.
Mungu kwa uweza wake alisababisha Maria angali bado bikira kupata mimba na kuzaa mtoto Yesu.
Imeandikwa katika maandiko,
muujiza wa kuzaliwa kwake, Ilikuwa ni ishara ya Mungu kwamba, mtoto huyu alikuwa Ni Masihi,
ambaye Mungu alimwita Mwanaye.
Watu walipomwona Yesu, waliona asili na uweza wa Mungu.
Aliponya watu na kuwasamehe dhambi zao. Na kuwaahidi mahali katika Ufalme wake.
Yesu alitoa maisha yake, na kupata mateso Kwa ajili ya watu wote.
Kisha, alifufuka akionyesha kwamba uwezo wake ni mkubwa kuliko uwezo wa mauti.
Yesu Masihi alisema: Nina uwezo wa kuutoa uhai wangu, na uwezo wa Kuutwaa tena.
Maisha ya Yesu yalikuwa kama manabii walivyo andika kawmba, Masihi angekuwa.
Kweli, Yesu ni Neno la Mungu. Katika Yesu Mungu anajionyesha mwenyewe kwa watu wa ulimwengu huu.
Yesu Masihi alisema: Mbingu na dunia vitapita lakini maneno yangu hayatapita kamwe.
Hapo mwanzo Mungu alimumba mwanaume na mwanamke ili kwamba wangeishi na furaha kwake.
Lakini hawakumwamini Mungu na kutii amri zake. Kitendo hiki cha aibu kiliwatenganisha wao na Mungu.
Katika maandiko imeandikwa; Wote wamefanya dhambi, na mshahara wa dhambi ni mauti.
Watu waliofanya dhambi hawawezi kuishi katika uhusiano pamoja na Mungu.
Kama Mungu alivyo mtowa kondoo kufa badala ya mtoto wa Abrahamu,
Ndivyo Mungu alimtuma Yesu ili afe badala ya uzao wa Adamu.
Alifanya hivi ili wale wote ambao wanamwamini, nakuweka imani yao katika Bwana Yesu.
Waweze kwenda katika uwepo wake.
Petro alisema; Yesu ni yule ambaye manabii walitabiri.
Wakisema kwamba Mungu atasamehe dhambi za kila mtu atakaye mwamini.
Kwa hiyo, wale wamfuatao Yesu, wataepuka hukumu na wataishi na Mungu milele.
Wakati Yesu amefufuka kutoka wafu, alisema kwa wamfuatao: Watu watatangaza katika jina langu kwa mataifa yote,
Kwamba Mungu anasamehe dhambi, kwa wale wanaomgeukia Na kutubu.
Yesu alisema pia: Angetuma Roho Mtakatifu kwa wanafunzi wake ili kuwaonyesha kweli
na kuwapa uwezo wa kufuata njia ya Mungu.
Wakati mwanamke mwenye dhambi alipotubu dhambi zake Na kuanza kumfuata, Yesu alisema kwake:
Umesamehewa dhambi zako. Umeokolewa kwa sababu umeniamini.
Yesu alisema; watu wanapompenda Mungu kweli, Ni ushahidi kwamba Mungu amewasamehe dhambi zao.
Yesu Masihi aliwaita watu wamfuate.
Wakati mhalifu pale msalabani alimwamini Yesu Na kuomba kuokolewa, Yesu alisema:
Leo hii utakuwa nami peponi.
Wale ambao wanaamua kumfuata Yesu, Wanaweza kuanza uhusiano wao naye kwa Kutumia sala kama hii;
Mungu Baba, wewe ni mwenye haki. Nakushukuru kwamba unanipenda.
Najuta kwamba nimetenda dhambi, na kutotii amri zako.
Nashukuru kwamba ulimtuma Yesu kufa, Msalabani kwa niaba yangu. Na kwamba akafufuka toka kwa wafu.
Nakushukuru kwamba aliumia kwa adhabu Ya dhambi nilizozifanya.
Ninakupokea Yesu kama Bwana na Mwokozi wangu.
Nakushukuru kwamba umenisamehe dhambi zangu.
Na umefungua njia kwa ajili yangu, kuwa nawe daima.
Nakuomba unipe Roho Mtakatifu wako, awe nami Na kunionyesha njia yako.
Anipe uwezo ili nikupende wewe kwa moyo wangu wote. Na kuisha maishi yanayokupendeza.
Na watu waweze kukusifu wewe popote Ulimwenguni. Amen!
Yesu alisema kuhusu wamfuatao; Kondoo wangu waisikia sauti yangu, nami Nawajua, nao wanifuata.
Wamufuatao Yesu hukutana pamoja, Wanazungumza naye kila siku. Wanajifunza neno lake katika maandiko.
Wanatafuta kufuata mfano wake. Na wanawaambie wengine kuhusu Yeye.
Yesu huwasaidia wao na kuwatia nguvu kupitia uwezo wa Roho wa Mungu, ambaye anaishi ndani ya mioyo yao.
Wanaweka mioyoni mwao, yale Yesu aliyoyasema, Wakati akipanda juu kwenye kiti chake cha enzi mbinguni.
Mungu amenipa mamlaka yote mbinguni na duniani.
Kuwa na hakika na hili, nami nipo pamoja Nanyi daima hata mwisho wa ulimwengu.