10 kati ya 59Women's Resources · 59 sura

Magdalena - Director's Cut

Magdalena, a film made especially for women, beautifully shares God's love and the gospel, engaging women at the heart level with the potential of changing their lives for eternity. A story of tenderness, freedom and purpose, it portrays Jesus' compassion for women and historical accounts of His interactions with them, as seen through the eyes of Mary Magdalene.

Uliza lako

Nukuu za Biblia

Shiriki
Rasilimali Bure

Ungependa kuelewa Biblia kwa kina zaidi?

Jiunge na masomo yetu ya Biblia

Nakala

Swahili, Tanzania (Kiswahili)
Simulizi ifwatayo inatokana na mashuhuda ya maisha ya Yesu Kama ilivyo andikwa kwenye injili ya mtakatifu Matayo, Marko, Luka, na Yohana. Imesimuliwa na Maria Magdalena ambaye maandiko yana mtaja kama mmoja wa wafuasi wa Yesu. Simulizi yake yenye kuvutiya na usahihi imeeleza hadisi ya kweli, ya mtu aliyeishi karibu myaka 2.000 iliyo pita. Muigizaji anaye husika sehemu ya Yesu, japo kuwa hakuna muigizaji anaye faa kwenye nafasi hii, Imefanywa hivyo ilituweze kuelewa na kufaidika kutokana na maisha ya Yesu. Nardine Productions Ikishirikiyana na Inspirational Films, Inc. wanatuonyesha Magdalena akifunguliwa kutoka katika aibu Palestine 40 A.D. Eee! huku huwezi kuniona mimi, ebu tuone kama uta nikamata! niko huku! (Kicheko) Huwezi kunikamata! niko huku! ebu nikamate! Ahaa! Angalia! Ni nzuri namna gani kazi atuonyeshayo Mungu kila siku jioni. Inanikumbusha upendo wake mkubwa kwa ajili yangu. Na kwako. Mungu aliumba vyote hivi? Nina shaka kama ananiona na mimi Hani juwi hata kidogo. Huenda Mwenyezi Mungu ange mpenda mtu mtakatifu Lakini si mtu kama mimi Rivka, laiti unge kuwa na mimi wakati huo wa myaka mitatu aliyo tufundisha. Mwalimu, Yesu? Safira. Unge penda ku tuambia habari zake? Ndiyo, tafathali tuambiye hadisi yake Ndiyo, nta waambia, Karibu. Vyema Lazima tuanziye mwanzo kabisa. Ulipo kutana na Yesu? Subiri, ili kufahamu hadisi ya Yesu, lazima tuanziye mwanzo kabisa. Kama maandiko matakatifu yanavyo tu fundisha. Hapo mwanzo, Mungu aliumba dunia na mimeya yote, wanyama, ndege, na viumbe vya baharini. Tokana na udongo, alimfanya mtu wa kwanza. Na aka mpulizia pumzi ya uhai katika puwa zake. Mtu wa kwanza aliitwa Adamu. Mungu aka sema, "Si vema mtu huyo awe peke yake. Nita mfanyia msaidizi wa kufanana naye." Kisha Mungu aka towa ubavu wa Adamu, na ku tokana na huo, alimfanya mwanamke aitwaye Eva. Si toka kichwani mwake, ili amtawale, Wala si toka miguuni ili amkanyage, Bali kutoka ubavuni ili awe sawa naye. Chini ya mkono ili amlinde, Na karibu na moyo wake ili ampende. Mungu wa upendo alimuumba mwanaume na mwanamke kuonyesha mfano wake na kuishi kwa utulivu naye. Aliwapa mamlaka ku tawala viumbe vyote pamoja. Adamu na Eva waliishi katika uwepo wa Mungu katika bustani nzuri aliyo waandaliya, Iliyoitwa Edeni. Mungu alitembea na ku zungumza pamoja nao bustanini. Na ha kukuwa na mateso, manyanyaso, wala mauti. Mungu ali mwambiya Adamu, "Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula Walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile. Kwa maana siku utakapo kula matunda ya mti huo, utakufa hakika." Lakini siku moja Shetani alimjaribu Eva. Mwanamke aka lichuma lile tunda akala. Kisha aka mpa piya mumewe, aliyekuwa naye, naye akala. Tendo la aibu la Adamu na Eva la kutotii, liliharibu utulivu wa bustanini. Utulivu kati ya mwanamume na mwanamke, Na mapatano kati ya Mungu na wao. Mwanaume alilaaniwa na maisha ya taabu. Na mwanamke aliongezewa uchungu wa kuzaa na ku tawaliwa na mumewe. Lakini Mungu aliweka ahadi piya: kwamba siku moja uzao wa mwanamke, Uta mponda nyoka kichwa. Katika maandiko matakatifu, Mungu mwenye huruma Ana zungumuza juu ya mpango wa kurejesha utulivu na heshima kwa uumbaji wake. Alifunuwa sehemu ya mpango huo kwa nabii Abrahamu. Abrahamu ali mwamini na kumheshimu Mungu. Mungu ali muahidi kumbariki na ku wabariki watu wa mataifa yote kupitiya yeye. Ali ahidi ku uzidisha uzao wake, Kama mchanga uliyoko puani, na kama nyota zilizo angani. Abrahamu alimwamini Mungu. Hivyo alimwinuwa Abrahamu kama mmoja wa watumishi wake wenye haki. Na akamwita rafiki wa Mungu. Siku moja, Mungu alimpa mtihani Abrahamu. Alimwambiya Abrahamu amchukuwe mtoto wake na amtowe sadaka. Abrahamu alijuwa kwamba kupitiya mtoto huyu, Mungu aliahidi kumpa uzao mwingi, Na kubariki mataifa yote, hata hivyo alimwamini Mungu na kumtii. Mungu aliita “Abrahamu!” "Sasa najuwa kuwa unanitii, kwa kuwa huku nizuwiliya mwanao mwana wako wapekee." Abrahamu akaangaliya kando akaona kondoo. Aka mtowa awe sadaka ya kuteketeza badala ya mwanawe. Mungu kumu patiya Abrahamu kondoo badala ya mwanawe ilikuwa ni ishara... dokezo la mpango wake mkubwa. Mpango huu unge haribu laana ya dhambi na mauti Na kuwa rejesha wanaume na wanawake kwenye uhusiano wa karibu naye. Maandiko matakatifu husema kwamba huyo ajaye Ndiye atakaye kuwa sadaka ya mwisho ya dhambi za ulimwengu. Manabii walimwita mtu huyu "Masihi." Kuja kwake kunge leta baraka kubwa kwa maana ange kuwa ndiye Mwokozi, Nabii, na Mfalme. Isaya alielezeya nini Masihi ange fanya wakati atakapo kuja. Mpakwa mafuta wa Bwana ataleta habari njema kwa maskini, ataponya waliyo vunjika moyo, Kutangaza kufunguliwa kwao waliyo fungwa, na uhuru kwa waliyo kifungoni. Na kutangaza wakati muafaka wa Bwana kuokowa watu wake. Mwalimu alitembeya hapa duniani aliitwa Yesu. Je? ndiye aliye tumwa na Mungu kumponda kichwa nyoka? Kuleta nuru kwa ulimwengu wetu wa giza na ku badilisha laana kuwa baraka? Je? yeye angeweza kuwa ndiye Masihi mtarajiwa? Je? ange weza kumkombowa yule anaye jisikiya woga, au aibu, au kuto thaminiwa? Kuli kuwa na msichana aliyeishi Nazareti ambaye alipozwa na mtu aliyeitwa Yosefu. Jina lake aliitwa Mariya. Bwana yu pamoja nawe na amekubariki sana! Usi ogope, Mariya. Kwa maana ume pata neema kwa Mungu. Uta beba mimba na kupata mtoto wa kiume Na uta mwita jina lake Yesu. Lakini mimi ni bikira. Inawezekanaje? Roho Mtakatifu atakujiliya, na nguvu za Mungu zitakufunika. Mtoto utakaye mzaa atakuwa mkuu na ataitwa Mwana wa aliye juu. Hata Elizabeti jamaa yako atapata mtoto katika uzee wake, Na mwezi huu ni wa sita kwake yeye aliyeitwa tasa. Kwa kuwa hakuna lisilo wezekana kwa Bwana. Mimi ni mtumishi wa Bwana. Na iwe kwangu kama ulivyosema. Ndiyo Mariya aka ondoka kwa haraka ku mtembeleya binamu yake Elizabeti. Elizabeti! Mariya! Binamu Mariya! Oh, ni kweli. Lakini wewe ume barikiwa katika wanawake wote. Naye uzao wa tumbo lako ame barikiwa. Lime tokayaje kwangu jambo hili kubwa hivi Hata mama wa Bwana wangu anitembeleye mimi? Nilipo sikiya sauti ya kuamukiya kwako Kitoto kikaruka kwa shangwe tumboni mwangu. Moyo wangu wa mwadhimisha Bwana; Na roho yangu imemfurahiya Mungu mwokozi wangu, kwa kuwa amenikumbuka mtumishi wake, Tokeya sasa vizazi vyote vitaniita "mbarikiwa." Mariya alikaa na Elizabeti kwa myezi mitatu. Wakati Yosefu alipo tambuwa mke wake wa ahadi ana mimba, aliazimu kumwacha kwa siri. Lakini Mungu aka mtuma malaika kwa Yosefu katika ndoto. Usihofu kumchukuwa Maria mkeo. Maana mimba yake ni kwa uwazo wa Roho Mtakatifu. Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu. Kwa sababu ndiye atakaye waokowa watu wake na dhambi zao. Hivyo Yosefu akamchukuwa Mariya kuwa mkewe. Yesu alizaliwa Bethlehemu mahali pa kuliya ngombe, Kwa kuwa Mariya na Yosefu hawa kupata nafasi katika nyumba ya jamaa zao. Kuli kuwepo malaika wengi waliotangaza kuzaliwa kwake. Wakati ulipowadiya wa mtoto kutahiriwa, alipewa jina Yesu, Ambalo lina maana "Mungu ana okowa." Mariya na Yosefu walikwenda na mtoto hekaluni ili kumkabidhi mbele za Bwana. Nabii aitwaye Simiyoni alikutana nao. Mtoto huyu ame chaguliwa na Mungu Kwa kuanguka na kuinuliwa kwa walio wengi. Atakuwa ishara toka kwa Mungu. Ambaye watu wengi wata nena kinyume chake Na kufunuliwa mawazo ya siri ya mioyo yao. Na huzuni Kama upanga mkali Itaingiya moyoni mwako. Nilipo sikiya hadisi yake, nilijuwa Yesu ange kuwa zaidi ya nabii wa kawaida. Malaika alikuwa na maana gani alipomwita Yesu "Mwana wa aliye juu?" Hakika, huna maana kwamba Mungu alikuwa na uhusiano na mwamke? Hapana! hapana, hapana. Kumbuka Mariya ali kuwa bikira. Mimba ya Yesu kweli ilikuwa ni muujiza kutoka kwa Roho wa Mungu. Mungu anaweza kufanya lolote. Je? huamini hili? Kwa sababu ya mwanzo wake wakimuujiza Yesu alizaliwa na mwanamke kama wewe na mimi. Hata hivyo alikuwa zaidi yetu. Tubuni dhambi zenu Na mkabatizwe Na Mungu ata wasamehe dhambi zenu. Mungu, mwenyewe, alisema hili wakati Yohana Mbatizaji mwana wa Elizabeti, Alipo kuwa anabatiza wanaume na wanawake katika mto Yorodani. Nawabatiza kwa maji. Lakini yuaja mtu mwenye nguvu kuliko mimi. Ambaye mimi sistahili hata kulegeza kamba za viatu vyake. Yeye ata wabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto. Ambaye ungo wake u mkononi mwake, atapepeta makapi na kukusanya ngano galani mwake. Na Roho Mtakatifu akashuka juu ya Yesu kwa umbo la huwa. Na sauti ika toka mbinguni na kusema Wewe ndiwe Mwanagu Mpendwa. Nime pendezwa nawe. Baada ya ubatizo, Yesu alisafiri kupitiya miji aki fundisha, Na ujumbe wake uli kuwa wa kuthibitisha mamlaka yake. Je? huyo si mtoto wa Mariya? Ndiyo, ni yeye, Nyamanza. "Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana ame nitiya mafutu kuwa hubiri maskini habari njema. Ame nituma kuwatangaziya wafungwa kufunguliwa kwao na vipofu kupata kuona. Kuwa acha huru walio nyanyaswa, Na kutangaza wakati muafaka wa Bwana kuwa okowa watu wake." Anena vema. Leo maandiko haya yametimiya masikioni mwenu Kama mlivyo yasikia yakisemwa Je? maandiko yametimiya? Lakini Masihi tu ndiye ana weza kutimiza ahadi hiyo! Tutafahamu vipi? Maneno yake yaliwashangaza wengi, Na miujiza yake ilisababisha wengi kuamini. Ni yeye. Anafanya tena. Ni nani huyo? Ni yule mwalimu toka Nazareti Yesu. Hujambo. Sijambo. Ondoka. Hutakiwi hapa. Mwalimu mwache huyo. Usijinajisi bure hata kwa kumwangaliya. Mariya. Unataka nini kwetu Yesu Mnazareti? Tuna kujuwa wewe ni nani Mtakatifu wa Mungu! Kaa kimya! roho chafu Toka kwa mwanamke huyu. Amekufa. Amemuuwa! Anataka kumgusa! Hapana! mtu mtakatifu hawezi kufanya jambo kama lile! Mariya Bintu wa Abrahamu. Ni mzima! Yuko hai! Ni muujiza! Mtu huyu ni nani? Hata pepo wana mtii! Ni muujiza. Ni muujiza. Inawezekanaje? Asante. Nashukuru. Nashukuru. Asante. Kuanziya wakati huo, nikawe mfuasi wake Nilitaka kufanya kinacho mpendeza Mungu. Kwa myaka mingi, niliishi katika aibu. Lakini Yesu ali rejesha heshima yangu. Nguvu yake iliwafukuza wale pepo wachafu. Uuuu, Safira! Dina! Ume sikiya Yesu akifundisha na umeona miujiza mingi aliyofanya. Ndiyo. Kwa hiyo unajuwa kwa nini niliacha kilakitu ili kumufwata yeye. Na sikuwa peke yangu. Kulikuwa na wafuasi wake: (Simoni) Petro Batolomeo Matayo Yuda (Isikariote) Na wengine waliobaki jumla kumi na mbili. Na wanawake: Suzana Yoana Mimi mwenyewe, nawengine waliyochangiya kila mmoja kutoka nyumbani mwake kuwa saidiya Yesu na wafuasi wake. Wote tulitumahi kwamba hatimaye Mungu amemtuma Masihi tuliye mtarajiya. Hakika tulimuhitaji Mwokozi. Roma ilitutawala kwa mkono wa chuma. Wali chukuliya kila kitu cha thamani na kutulipisha kodi kwa kidogo kilicho baki. Tulikuwa wenye njaa, kimwili na kiroho, na tulihitaji mtu mmoja wa kutu onyesha njiya ya Mungu. Baada ya myaka mingi ya mapambano na kukatishwa tamaa, wengi wetu tulikosa tumaini. Bali Yesu alionekana kutowa tumaini popote alipokwenda. Nani-nani huyo? Kijana wa kiume. Mtoto pekee wa mjane. Kijana, inuka! Nabii mkuu ame tokeya katikati yetu! Mungu amekuja kuokowa watu wake! Heri ninyi mlio masikini Kwa kuwa Ufalme wa Mungu ni wenu. Heri ninyi mlio na njaa sasa, kwa sababu mta shiba. Heri ninyi mliao sasa, kwa sababu mtacheka. Heri ninyi watu watakapo wachukiya na kuwa tenga na kuwa shutumu Na kusema ni waovu, kwa sababu ya Mwana wa mtu. Furaheni siku ile na kurukaruka kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni. Kwa kuwa babu zao waliwatenda manabii vivyo hivyo. ...Kumi na saba, kumi na nane, kumi na tisa, ishirini. Ni hizo tu ninazo. Una maana gani hizi tu ndo ulizonazo! Ole wenu mlio na mali sasa! Kwa kuwa faraja yenu mume kwisha kuyipata. (Kicheko) Hataki utajiri huyu. Anabakizwa akili. Ole wenu mnao cheka kwa sasa Kwa kuwa mtaomboleza na kuliya. Ole wenu ninyi watu wote watakapo wasifu Kwa kuwa baba zao waliwatenda manabii wa uongo mambo kama hayo. Lakini nawaambiya ninyi mnao nikiya: Wapendeni adui zenu. Watendeeni mema wale wanao wachukiya. Wabarikeni wale wawalainio ninyi. Waombeeni wanao waudhi. Akupigaye shavu moja Mgeuziye la pili piya. Naye aku nyanganyaye koti lako, usi mzuwuliye na shati piya. Mpe kila akuombaye kitu. Akunyanganyaye vitu vyako Usitake akurudishiye. Kama mnavyotaka kutendewa na watu Nanyi watendeeni vivyo hivyo. Mki wapenda wale tu wanao wapenda ninyi Kwa nini mpokee baraka? Hata wenye dhambi wapenda wa wapendao Nanyi mkiwatendendeya mema wale wawatendeao mema Kwa nini mpokeye baraka? Hata wenye dhambi hufanya hivyo. Ana wezaje kumgusa? Ana wezaje kuzungumza naye? Inakera? La Wapendeni adui zenu Watendeeni mema. Na mkikopesha msi tumaini kurudishiwa. Ndipo mtapata thawabu kubwa Nanyi mtakuwa wana wa aliye juu. Kwa kuwa yeye ni mwema kwa wasiyo na shukurani na waovu. Iweni na huruma. Kama Baba yenu alivyo na huruma. Tuokowe, Yesu! Msihukumu nanyi hamta hukumiwa! Msilaumu Nanyi hamta laumiwa! Sameheni Nanyi mtasamehewa. Tuongoze katika njiya yako Bwana! Toeni vitu nanyi mtapewa. Kwa kuwa kipimo mpimiwacho ndicho mtakacho pimiwa. Mtu kipofu hawezi kumwongoza kipofu mwenziye! Akifanya hivyo wote wawili wata tumbukiya shimoni. Mbona wakiona kibanzi ndani ya jicho la ndugu yako Na boriti jichoni mwako hulioni? Tuongoze, eee! Bwana! Tuna kuhitaji sasa Bwana! Heri mama aliyekuzaa na matiti uliyo nyonya! Lakini heri yao wasikiyao neno la Mungu Na kulitii. Yesu alifundisha kwamba Mungu humtendeya mema hata mwenye dhambi nyingi si kama aduwi wa kumuangamiza, Bali kama kondoo aliye poteya ambaye humutafuta ili kumwokowa na kumurejesha kundini mwake. Hatu kujuwa maana ya hali ya kuwa thamini na kuwa penda watu hata wale tulio wadharau makarini nyingi, chotara wenye desturi za kigeni walione kama hawafai, Mpaka Yesu alipo chaguwa kusafiri kupitiya Samariya. Ni mwanamke gani huyu ambaye watu wana mudharau? Ni musamariya. Je? ubaya huu hautoshi? Twende zetu. Tunataka kununuwa chakula, hatutaki kumuacha mwalimu akisubiri. Je? utanipa maji ninywe? Wewe ni muyahudi. Mimi ni mwanamke musamariya. Unawezaje kuniomba mimi maji? Laiti unge lijuwa atowacho Mungu na ni nani akuambiaye nipe maji ninywe Ungeli mwomba yeye Naye angeli kupa maji yaletayo uzima. Bwana Huna kitu chakuchoteya maji na kisima ni kirefu. Utayapata wapi hayo maji ya uzima? Baba yetu Yakobo ndiye aliyetupa kisima hiki. Yeye wanawe na mifugo yake walikunywa toka kisima hiki. Je? wewe nimkubwa kuliko baba yetu Yakobo? Kila anywaye maji haya ataona kiu tena. Yeyote anywaye maji nitakayo mupa mimi Hataona kiu tena. Maji nitakayo wapa yata kuwa chemichemi ndani yao Yaki bubujika uzima wa milele. Bwana Unipe maji hayo! Ili nisione kiu tena Wala nisije hapa kuteka maji. Nenda kamwite mumeo na urudi hapa. Mimi... Mimi sina mume. Umesema vema unavyosema huna mume. Kwa maana umekuwa na wanaume watano. Na uliyenaye sasa siyo mume wako hasa. Hapo umeniambiya kweli. Bwana. Naona yakuwa u nabii, Baba zetu wasamariya walimwabudu Mungu katika mlima huu. Lakini nyinyi wayahudi husema Yerusalemu nimahali patupasapo kumwabudu Mungu. Mwanamke, niamini, saa inakuja Ambao hamuta mwabudu Baba katika mlima huu wala kule Yerusalemu. Nyiye wasamariya mnaabudu msicho kijuwa. Lakini saa inakuja Na ndiyo sasa Wakati kwa uweza wa Roho wa Mungu watu watamwabudu Baba kama alivyo, Wakifanya ibada halisi anayo taka. Mungu ni Roho, ni kwa uweza wa Roho wake tu watu wataweza kumwabudu yeye kama alivyo. Yule mwanamke Ana fanya nini anapo zungumza naye? Anamjuwa yeye ni nani? Najuwa Masihi atakuja. Na atakapo kuja, atatwambiya kila kitu. Mimi ndiye. Njooni mumuone yule mtu aliyeniambiya mambo yote niliyowahi kuyatenda. Njooni. Anaweza kuwa ndiye Masihi? Masihi? Masihi? Aliyeahidiwa (kuja)? (hapana) haiwezekani. Njooni mumuone. Njooni. Mwalimu, kula kitu! Mimi nina chakula msicho kijuwa. Je? kuna mtu amemuleteya chakula? Chakula changu Ni kuyatenda mapenzi yake aliye nituma Na kuyimaliza kazi yake aliyonipa. Mazao yame kwisha komaa Tayari kwa mavuno! Tazama wangapi wanakuja! Na habari njema kwa wasamariya, piya? Watu toka mjini walimujiya Yesu na kumusihi akae kwao na kuwafundisha. Tulikaa kwa siku mbili, na wasamariya wengi wakamwamini yeye. Ombeni, nanyi mtapewa; Tafuteni, nanyi mtaona; Bisheni, nanyi mtafunguliwa. Kwa kuwa kila aombaye hupokeya Nakila atafutaye huona Nakila abishaye mlango hufunguliwa. (kicheko) Na yupi aliye baba ambaye mwanaye akimwomba samaki atampa nyoka au atampa inge badala ya yai? Basi ikiwa ninyi mulio waovu, munajuwa kuwapa watoto wenu vitu vizuri. Je? Baba aliye mbinguni hata zidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao wamwombao. Na waambiyeni Msisumbukiye maisha yenu mutakula nini Wala miili yenu mtavaa nini. Kwa kuwa maisha ni zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi. Watafakarini kunguru: Hawapandi wala hawavuni, hawana gala wala kihenge Bali Mungu huwalisha. Je? ninyi si wathamani zaidi kuliko ndege? Yupi kwenu akijisumbukiya, anaweza kujiongezeya maisha yake? Ikiwa hamuwezi kujitendeya neno hilo ndogo kwa nini kujisumbukiya kwa yale mengine? Tafakarini mauwa, jinsi ya meavyo, Hayatendi kazi wala hayasokoti Hata Solomoni katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama hayo. Ikiwa Mungu Huvika hivi majani ya kondeni kesho hutupwa motoni Je? hata wavika ninyi zaidi? Enyi wa imani haba. Tuongezeye imani zaidi. Kama mungekuwa na imani kiasi cha punde la haradali, munge uambiya mti huu wa mkuyu Ngoka ukajipandikize baharini, nao unge watii. Makwazo hayana budi kuja. Lakini ole wake ambaye yaja kwasababu yake. Inge mfaa zaidi mtu huyo jiwe lakusagiya lifungwe shingoni mwake Akatupwe baharini, kuliko kumkosesha mmoja wapo wa wadogo hawa. Ufalme wa Mungu umefanana je? Uko namna hii: Mtu anaye twaa punje la haradali na kulipanda shambani mwake. Ikameya ikawa mti mkubwa ndege wa angani wakakaa katika matawi yake. Sina hakika anazungumziya nini. Kwa nini unakula na kunywa pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi? Wenye dhambi? Wenye afya hawahitaji dactari, isipokuwa wale ambao ni wagonjwa. Sikuja kuwaita wenye haki bali wenye dhambi wapate kutubu. Anakuja! huyu hapa! angaliya! Yesu! Yesu! Na kuomba mwokowe bintu wangu wapekee! Bwana, ni hurumiye. Ana myaka kumi na miwili tu na... anakufa. tafathali njoo nami! Nikiyagusa mavazi yake tu. Nitapata uponyaji. Samahani, Yairo. Yairo, usimsumbuwe mwalimu. Yesu! Binti yako amefariki. Usimsumbuwe mwalimu tena. Usiogope. Amini tu, na atapona. Ninani aliyenigusa? Kuna mtu aliyenigusa. Maana naona nguvu zimenitoka. Ni mimi niliyekugusa. Nimeteseka myaka kumi na mbili nikitoka damu. Nimetumiya mali zangu zote kuwapa waganga bila kupona. Lakini nilipogusa vazi lako tu Nika pona. Binti Imani yako imekuponya. Nenda kwa amani. Asante. Alimwita yeye "binti?" Ndiyo, mtu ambaye alikuwa najisi kwa myaka kumi na mbili kutokana na sheriya zetu. Aliona aibu yake na kumurudishiya heshima yake. Sijuwi nikipi kinacho leta uponyaji mkubwa hivi. Nguvu ya Yesu Au huruma yake. Usiliye. Hajafa huyu, bali amelala tu. Mtoto, Amka. Mupeni kitu chakula. Nisikilizeni Msimwambiye mtu kilicho tokeya hapa. Yuu hayi. Binti wa bwana, mwalimu amemrudishiya uhayi! Mungu apewe sifa! Yuko hayi! Habari zilizagaa kuhusu miujiza yake ya ajabu Na watu wengi zaidi na zaidi walianza kumufwata Yesu. Bwana Waage watu waende zao Ili waende katika vijiji na mashamba karibu Wakatafute chakula na mahali pa kulala hapa tulipo hakuna kitu. Ninyi wenyewe wapeni kitu chakula. Tulichonacho ni mikate mitano na samaki wawili tu. Uhimidiwe wewe, E Bwana Mungu wetu, Mfalme wa ulimwengu, utupaye chakula kutoka katika ardhi yetu. Nimuujiza. Unashangaza! Wote tulikula mpaka tukashiba, na tulipokusanya mabaki, Tulijaza vikapu kumi na mbili. Huu nimuujiza wa kushangaza unao tukumbusha baraka zinazo letwa na Yesu Kwamba tunapaswa kumufwata yeye. Nani kati yenu atanifwata? Nita kufwata Bwana Lakini kwanza, niruhusu niage wa nyumbani kwangu. Mtu aliyetiya mkono wake kwa kulima kisha akaangaliya nyuma hafai kwa ufalme wa Mungu. Mtu yeyote akitaka kunifwata, na ajikane mwenyewe Ajitwike msalaba wake kilasiku, na anifwate. Kwakuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake atayiangamiza Na mtu atakaye angamiza nafsi yake kwa ajili yangu atayiponya. Itamfaa nini mtu kuupata ulimwengu wote kama ataipoteza nafsi yake mwenyewe? Ikiwa mtu atanioneya haya mimi na maneno yangu Mwana wa mtu atamwoneya haya atakapo kuja katika utukufu wake Na utukufu wa Baba na wamalaika watakatifu. Nawaambiya kweli Wapo watu hapa ambao hawataonja mauti kabisa hata wauone kwanza ufalme wa Mungu. Msiogope, enyi kundi ndogo, kwakuwa Baba yenu anaona vema kuwapa ule ufalme. Viuzeni vyote mlionavyo muwape maskini. Jifanyiyeni mifuko isiyochakaa jiwekeyeni hakiba isiyopunguwa mbinguni, Mahali ambapo hazitapunguwa Mahali asipoweza mwizi kuzikaribiya. Wala nondo kuharibu Kwa kuwa niya yako ilipo ndipo utakapokuwapo na mayo wako, Mwanamke Umepona katika ugonjwa wako. Angaliya! angaliya, amepona! nimiujiza! angaliya, angaliya, amepona! njooni, muone! Muujiza mwingine! Si-si- si-sifa Kwa Bwana! Myaka kumi na nane! Mungu akulinde, Mwalimu! Kuna siku sita za kufanya kazi. Njooni kati ya siku hizo ili mponywe, lakini siyo siku ya sabato. Enyi wanafki! Yeyote kati yenu amfunguwe punda au ngombe wake zizini siku ya sabato? Aende naye kumnywesha maji, Nahapa yuko binti wa Abrahamu ambaye Shetani alimfunga myaka kumi na nane. Je? haimpasi kufunguliwa siku ya sabato? Watawala wa Roma na viongozi wetu wadini walishangaa waliomfwata Yesu. Nafahamu wengi wamemtukuza kuwa ndiye mfalme. Mfalme? Ha, ha, ha. Mfalme wa waombaji, wamalaya, na wezi. Tuliwahi kuwaona watu kama hao. Wanakuja, wanaleta madai yao, wanaondoka. Kisha wana sahaulika. Usiwe kipofu. Wanaomfwata wanaongezeka kila siku. Watu wanamuhusudu. ...na wanafikiri ni mfalme. Hebu niwatahadharishe. Ikiwa mtu huyu anatishiya amani zaidi, Nitawatazamiya ninyi. Huenda yuko sahihi. Nimuda wakumkabili huyu mugalilaya. Nikidogo sana. Sarafu mbili ndogo tu. Je? hawezi kutowa zaidi? Nawaambiyeni Mwanamke huyu maskini na mjane ametowa zaidi kuliko wote. Maana hawa wengine wametowa sadaka katika mali ilyowazidi. Bali huyu, katika umaskini wake, ametowa vyote alivyonavyo vinavyo muwezesha kuishi. Tuambiye: Unatenda mambo haya kwa mamlaka gani? Tena nani aliyekupa mamlaka hii? Hebu niwaulize swali. Niambiyeni, ubatizo wa Yohana ulitoka kwa Mungu au kwa watu? Hatujuwi imetoka wapi hii. Wala nami siwaambii kwa mamlaka gani natenda haya. Lakini badala ya kutambuwa huruma ya Yesu, Wale waliokinyume naye walitafuta namna ya kumushitaki. Mwenye dhambi! Mzinzi! Mzinzi! Kahaba! Mzinzi! kahaba! Mwalimu Mwanamke huyu tumemshika katika tendo la kufanya uzinzi. Katika sheriya zetu, Mose alituamuru Kwamba mwanamke kama huyu apigwe mawe hadi kufa. Ndiyo, apigwe! Kahaba! apigwe! Ndiyo, apigwe mawe! apigwe mawe! Kahaba! apigwe mawe! Apigwe mawe! Wewe wasema je? Mwalimu, sisi tuna ushahidi wa watu wawili. Tufanye nini na mwanamke huyu? Mwanaume yuko wapi? Sheriya inasema anatakiwa ashitakiwe piya. Yeyote kati yenu ambaye hajawahi kutenda dhambi, naawe wa kwanza kumtupiya jiwe. Mwanamke Wako wapi wale? Je? kuna aliyebakiya kukuhukumu? Hakuna, Bwana. Wala mimi sikuhukumu piya. Nenda sasa, na uache maisha yako ya dhambi. Tafathali niinuwe. Haya panda begani mwangu. Je? unaweza kuona sasa? Namuona Yesu. Anaasi sheriya. Mpanzi alikwenda kupanda mbegu. kwa kuvunja sabato zingine zilianguka karibu na njiani zikakanyagwa. Akishiriyana na wenye dhambi. Tukimwacha hivi hivi Watu wote watamwamini Watawala wa kiroma watachukuwa hatuwa ya kuharibu hekalu letu. Walishindwa kumnasa Yesu au kupunguza wafuasi wake, Lakini waliazimiya ku simamisha madai yake kuwa yeye ni Masihi. Nawalimpata mtu mmoja aliyetayari kumsaliti. Maranyingi Yesu aliwapeleka wafuasi wake mlima wa mizeetuni ili kuomba. Usiku ule alisumbuka sana rohoni. Mbona mmelala? Amkeni Muombe msije mukaingiya majaribuni. Yuda Ni kwa busu unamsaliti mwana wa mtu? Bwana, Je? tuwapige kwa upanga? Mkamateni. Yatosha! Je? ninyi mmekuja na mapanga na marungu kunikamata kana kwamba ni myanganyi? Nili kuwa nanyi siku zote hekaluni na hamu kunitiya nguvuni. Lakini huu ni wakati wenu wa kutenda Wakati wa nguvu za giza kutawala. Mkamateni! Rafiki yake amemsaliti? Mmoja wa wafuasi wake? Mtu ambaye tulimfahamu kweli na kumwamini. Mlindeni vema. Usiku ule, walinzi walimdhihaki na kumpiga. Nani amekupiga? Tabiri! Nani atakupiga tena? Acha! Acha, nasema! Aletwe mbele ya baraza. Tuambiye Je? wewe ndiye Masihi? Hata nikiwaambiya Hamtanisadiki. Nahata kama nikiwauliza swali hamta nijibu. Lakini tangu sasa Mwana wa mtu atakuwa ameketi upande wa kuliya wa Mungu mwenyezi. Kwa hiyo wewe, Ni Mwana wa Mungu? Wewe wasema mimi ndiye. Anena kufuru! Je? kunahaja ya ushahidi mwingine? Nani amempa mamlaka kunena haya? Sasa mmesikiya kukufuru kwake! Hatiya! Sisi wenyewe tumesikiya kile alichosema. Anahatiya na anastahili kufa! Tutampeleka kwa Pilato. Ndiyo, ndiyo, mwondowe! Kwahiyo wakampeleka kwa gavana wa kiroma, Pontiyo Pilato. Kiongozi mkatili, aliyeitwa Pilato alihusika kusulubiwa kwa maelfu ya watu. Munataka nini hapa, asubuhi yote hii? Tumemkamata mtu huyu akipotosha watu wetu. Alileta gasiya katika soko la hekalu. Tumemuona ana hatiya, akiambiya watu wasilipe kodi kwa Kaisari, akidai yeye ni Masihi, Mfalme. Mfalme? Je? wewe ni mfalme wa wayahudi? Wewe wasema. Hatuna mfalme mwingine bali Kaisari. Tuna sheriya, na kwa sheriya yetu anastahili kufa, kwa sababu yeye alidai ni Mwana wa Mungu. Mtu huyu Haja fanya jambo linalostahili kifo. Kwa hiyo nitampeleka achapwe Nanita mwachiliya. Kama ukimwachiliya, wewe si rafiki wa Kaisari! Msulubishe! Ndiyo, msulubishe! Wewe, wewe, mchape. Kila mtu anayejidai kuwa mfalme anaasi kinyume cha Kaisari. Unangojeya nini, Pilato? Mwondowe huyo! muuwe! msulubishe! Hajafanya lolote baya. Mtu wa kufuru! auwawe! Hajafanya lolote baya! Kwa nini mnamtesa hivyo? Muacheni huru! Msulubisheni! Msulubisheni! msulubisheni! Nyuma! Rudi nyuma! Nyuma! Rudi nyuma! Ondoka njiana! Kaa mbali naye! Rudi nyuma! Rudi nyuma! Ondoka! Towa nafasi! Ondoka! Wewe, Pisha njaya! Sogeya na kwambiya! Amuka! Wewe! Jina lako nani? Simoni wa Kereni, bwana. Njoo hapa! Kata kamba! Wewe, beba. Haya, tembeya! Nyuma! Nyuma! Mwache! Nyuma! Rudi nyuma! Tunakuliliya wewe, Bwana, tunakuliliya. Kunywa, kunywa. Ndiyo, Kunywa, Bwana. Enyi wanawake wa Yerusalemu Msinililiye mimi Bali jililiyeni nafsi zenu na watoto wenu. Ikiwa mambo kama haya yanatendeka kwa mti mbichi Itakwaje ukiwa mti mkavu? Mungu akusaidiye. Tutakuombeya Inuwa msalaba! Wasamehe, Baba Kwakuwa hawajuwi watendalo. Alituokowa sisi; Ebu ajiokowe mwenyewe. Ndiyo, jiokowe mwenyewe ikiwa wewe ni Masihi! Shuka msalabani. Tuonyeshe mmoja wa miujiza yako! Mtu yeyote atundikwaye juu ya mti amelaaniwa na Mungu. Huzuni, kama upanga mkali, utanichoma moyo wangu... Na huzuni Kama upanga mkali Itaingiya moyoni mwako. Lakini, kwa nini? Je? Wewe ni Masihi? Jiokowe wenyewe Na sisi. Je? hu mwogopi Mungu? Tumepata hukumu moja Kama yeye Lakini Hajafanya kosa lolote. Nikumbuke, Yesu Uta ka--po ingiya katika ufalme wako. Nakuahidi Leo hii tutakuwa paradizo pamoja. Nami. Ilipo fika adhuhuri, anga likawa giza kwa saa tatu. Baba Mikononi mwako Nayiweka roho yangu Utukufu kwa Mungu hakika mtu huyu alikuwa mwenye haki. Ali kuwepo mtu moja wa baraza la kidini alikuwa mwenye haki ambaye hakushiriki katikakumu hukumu Yesu. Jina lake iliitwa Yosefu wa Arimatheya. Alipata kibali kutoka kwa Pontiyo Pilato Kuuweka mwili wa Yesu katika kaburi la karibu kwakuwa sabato ilianza panapo machoo ya juwa. Samahani. Tunaufwata mwili wa Bwana wetu. Karibuni nyote. Lakini njooni Sabato inakaribiya. Kwa nini waliamuwa kumuuwa? Ikiwa alitoka kwa Mungu, kwa nini aliruhusu wamuuwe? Niliulizwa maswali hayo yote. Yesu alikuwa na uwezo juu ya pepo wabaya. Hata na wafu walimsikiliza Je? asingezuwiya hili? Nilimufwata kwa myaka mitatu nikitegemeya kuwa ndiye Masihi aliahidiwa Lakini sasa ameondoka. Naninge kwenda wapi? Hadisi hii niya kusikitisha. Lakini, inamwisho wenye utukufu. Asubuyi ya juma pili, siku ya tatu baada ya Yesu kusulubiwa, Tulikwenda kaburini tukichukuwa manukato tuliyo andaa kwa kuupaka mafuta mwili wake. Jiwe limeviringishwa mbali. Petro... Yakobo... Yohana... sikilizeni. Jiwe limeviringishwa mbali! Tuliingiya, lakini mwili wa Bwana wetu haukuwepo. Wamemwondowa Bwana kutoka kaburini, na hatujuwi wapi wamempeleka! Nini? mwili wa Bwana wetu, haupo? Nenda ukajioneye mwenye. Baada ya kulichunguza kaburi, Petro alirudi kwa wanafunzi wengine. Lakini mimi nilibaki inje ya kaburi, nikiwaza, na kuliya. Lazima askari wamemchukuwa Au mafarisayo. Waliviuwa vyote tuvyo tumainiya. Angalau wange tuachiya mwili wake tu. Mwanamke, kwa nini unaliya? Wame mchukuwa Bwana wangu Na sijuwi wamempeleka wapi. Mwanamke, kwa nini unaliya? Ni nani ambaye unamtafuta? Bwana Kama ulimchukuwa wewe Niambiye wape ulimpeleka, ili niende nikamchukuwe. Mariya. Mwalimu! Usinishike kwa sababu sijapaa kwenda kwa Baba. Uko hayi, Bwana! Nenda, kawape habari hii ndugu zangu. Hujatusahau sisi, Mungu hajatuacha. Waambiye. Nime mwona Bwana! Nime mwona Masihi! Amefufuka? Ndiyo. Ki vipi? Mauti haikuweza kumshika. Sasa kwa nini ilimpasa kufa? Ili kushinda mauti. Ah, mimi sikuelewa siku ile, Lakini Yesu alitutokeya mara nyingi baada ya hapo Na akatufundisha. Mamiya ya myaka kabla ya Yesu kuja, Manabii walitabiri katika maandiko kwamba Masihi aliyeahidiwa angeteseka. Isaya ameandika, "Alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, na kwa kupigwa kwake sisi tumepona." Nabii Mose alisema, "Amelaaniwa na Mungu yeye aliyetundikwa juu ya mti." Yesu alipo kufa msalabani, ali chukuwa juu yake mwenyewe laana - laana yangu - ya dhambi, na mauti. Kujitowa kuwa sadaka na kufufuka kwake vimetuweka huru na kifungo cha uovu, Ametuokowa toka nguvu za giza, na kutukombowa tokana hofu ya maisha na aibu. Baraka hii ndiyo Mungu alimuahidi Baba yetu Abrahamu, Aliposema kuwa watu wote wa duniya watabarikiwa kupitiya yeye. Watu wote? Hata wanawake? Yesu aliniita mimi "binti wa Abrahamu." Wewe ni binti unayependwa binti ambaye anatakakubariki Kama mwanamke yule aliyemponya kutoka kuvuja damu myaka kumi na mbili... Au kama mimi. Hakuna kati yetu anayestahili kuishi katika hofu na aibu. Hatupaswi tujisikiye tena hatuonwi wala hatusikiwi. Yesu alijineneya mwenye: "Roho wa Bwana yu juu yangu Kwa maana ametiya mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwa tangaziya wafungwa kufunguliwa kwao na vipofu kupata kuona Kuwaacha huru waliyonyanyaswa Na kutangaza wakati muafaka wa Bwana wa kuwaokowa watu wake." Yesu aliwagusa watu, hata wanawake waliyoshambuliwa na magonjwa ingawa walihesabiwa kuwa najisi Na aliwaponya. Alifundisha watoto, wanaume na wanawake, tajiri na maskini, wenye haki na wenye dhambi, kuwarejesheya utu wao Na kudhihirisha huruma zake nyingi. Aliwaponya watu Akiwatowa pepo, akiwaweka huru wanaume, wanawake, na watoto kutoka vifungo vya Shetani. Hii inadhihirisha mamlaka yake juu ya pepo wabaya na kila roho. Yesu aliwarudishiya uhai wana na mabinti waliyo kufa Akionyesha anauwezo Hata juu ya mauti. Na ingawa Shetani na roho chafu waliamini walifanikiwa kupata ushindi wakati walipo mtundika Yesu msalabani, Yesu alifufuka kutoka ufuni, akishinda juu ya nguvu zote za uovu na mauti. Kwahiyo alikuwa Masihi? Ni Masihi tu aliyeahidiwa aliyetumwa na Mwenyezi Mungu angeweza kufanya miujiza ambayo Yesu alifanya. Ni mtu mwenye huruma tu, na uwezo, na kuaminika kama Yesu anastahili kuaminiwa na kuabudiwa nasi. Mungu alipoumba ulimwengu, Alimfanya mwanaume na mwanamke waishi katika uwepo wake na kupata furaha yake. Huo ndio ulikuwa mpango wake. Lakini hatukumwamini, na hatukutii amri yake. Tendo hili la aibu lilitutenganisha na Mungu, na kuharibu uhusiyano wa karibu kati ya mwanamke na mwanaume. Nasisi, piya, tumeendeleya katika uasi huo. Maandiko yana sema, " Hakuna mtu asiyetenda dhambi." Matokeo ya dhambi hii ni mauti na kutengana na Mungu. Lakini Mungu hakuridhika kuona sisi tunabaki tumetengwa naye na upendo wake, tukiishi kwa aibu na hofu. Hivyo, kama alivyotowa kondoo kufa badala ya mtoto wa Abrahamu, Mungu alimtuma Yesu kufa badala yetu. Maisha ya Yesu, kufa, na kufufuka kwake kulirejesha uhusiyano kati ya Mungu Na wale wanaomgeukiya na kumufwata. Na uhusiyano huu wa karibu na Mungu mwenyezi haukomi, hata tukifa. Muhalifu pale msalabani, alipokaribiya kufa, alimwamini Yesu... Na Yesu alimuahidi, " Leo hii utakuwa nami paradizo." Wale wote wanao weka tumaini lao kwa Yesu wataepuka adhabu ya milele na kuishi na Mungu milele. Inakuwaje? Kwakumufwata yeye kwa imani. Lakini atanikubalije mimi? Alimkubali Mariya na mimi. Nitajuwaje? Mwamini. Mwombe. Zungumza naye. "Mungu, Baba wa mbinguni U mtakatifu na wa haki. Asante kwa kunipenda. Nime kutenda dhambi. Asante kwa kumtuma Masihi aliyeahidiwa, Yesu Ilikuharibu laana ya aibu na hatiya. Nashukuru kuwa alikufa kwaajili yangu. Ninataka kumufwata mwokozi wangu aliye hayi. Nakushukuru kwa kunisamehe na kuni kubali mimi. Amina. Amina. Amina. Asante. Asante. Yesu alisema, "Kondoo wangu Waisikiya sauti yangu. Nami nawajuwa nao wanifwata." Anakujuwa, Rivka na anakupenda. Huu ni mwanzo wa uhusiyano wa milele Ambao unakuwa Tunavyo zidi kumujuwa zaidi na kumutumaini zaidi. Tunakuwa tunapolitii neno lake na kumwomba kwa imani Nakuwa pamoja na wamufwatao. Na kuwaambiya wengine kuhusu yeye, na kuyazingatiya tuliyoambiwa na Yesu: Bwana awabariki na kuwa linda. Mamlaka yote mbingu na duniani nimepewa mimi. Basi nendeni, mkayafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, Mtabatiza kwa jina la Baba, na la Mwana, na Roho Mtakatifu, na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi. Natazama mimi nipamoja nanyi sikuzote, hata mwisho wa ukamilifu wa ulimwengu.
JesusFilm