Inapakia video
Nakala
Swahili, Tanzania (Kiswahili)
Kanisa ni nini? Na kwa nini ni la muhimu sana?
Ingawa kanisa linafikiriwa kuwa mahali ambapo watu hukutana,
Mungu anasema kanisa ni kila mtu aliye Mali ya Yesu.
Hatukuokolewa na Mungu kwaajili ya kujitegemea
bali kumtegemea yeye na wengine wanaompenda.
Mungu anatamani kutufanya kuwa watumishi wasafi sisi kwa sisi,
katika jamii maalum inayompenda kuliko kitu kingine chochote.
Kama kanisa lake, tunafundishwa na Roho wake
na Neno,
jinsi ya kupendana na kusaidiana.
Na tunapokutana pamoja mara kwa mara ili kujifunza Biblia,
kuomba,
na kumwabudu Mungu,
tunasaidiana kukua na kustawi katika nyakati zote za furaha,
na huzuni.
Kwa kuishi pamoja kama familia ya Mungu, tunapata wengine wanaoweza kushiriki shida zetu,
na kututia moyo kuishi jinsi Mungu anavyotaka tuishi.
Hili linatupatia msaada wa ujasiri wa kueleza Wema wa Yesu, haki, msamaha na Upendo na dunia
Kwa njia hii, kanisa ni sehemu nzuri, na ya muhimu, ya maisha, ambayo Mungu amepanga kwa ajili yetu.