Inapakia video
Nakala
Swahili, Tanzania (Kiswahili)
Je, tunaanzaje kumwelewa Mungu wa ulimwengu mzima?
Hapo mwanzo Mungu alipowaumba watu wa kwanza na kuwaweka katika bustani nzuri.
alitembea nao, na kuwafundisha kibinafsi.
Mpaka maamuzi yao maovu yalipowatenga na upendo na uwepo wake.
Walakini watu hawakuishi bila tumaini.
Kwa sababu katika historia nzima, Mungu aliendelea kusema na waliompenda na kumtumikia,
na nyakati fulani, aliwaamuru kuandika na kuhifadhi yale aliyowafundisha.
Maandiko hayo yaliwekwa katika mkusanyo wa vitabu 66 vinavyoitwa Biblia.
Kupitia kusoma vitabu vya Biblia, tunaanza kuelewa Mungu ni nani, na ameahidi nini.
Pia, tulikotoka, sisi ni akina nani, na kusudi letu ni nini.
Kwa sababu tu ya mwongozo wa Biblia wa maisha mazima tunaweza kukua kumfahamu,
na kupata uhuru na maisha ambayo hayataisha.