Inapakia video
Nakala
Swahili, Tanzania (Kiswahili)
Ni kitu gani kuhusu damu ya Yesu, ambacho pekee kinaweza kuleta uzima wa milele?
Mungu alituambia kwamba uhai wetu uko katika damu yetu
Alituonya kwamba tusipomtii, tutakufa.
Lakini tulifanya hivyo.
Tulijaribu sana kubadili kile kilichokua ndani yetu,
Kwahio uwovu ukasambaa na kututawala.
Vurugu ilileta vurugu zaidi.
Uovu ulisababisha uovu zaidi.
Mungu alipotuona, udhalimu na jeuri vilimkasirisha.
na kumuvunja moyo
Kwa hiyo, aliahidi kwamba siku moja mtu maalum atakuja kuweka kila kitu sawa.
Kuna watu waliotarajia mfalme mkuu.
Wengi walijiuliza kama angewaua watu wote waovu.
Badala yake, kwa upendo, Mungu alijituma kama mtoto asiyejiweza.
Alikua na kuishi,
pamoja nasi,
kufa badala yetu,
kuuawa na sisi.
Kwa sababu ni damu ya mtu safi, asiye na hatia tu,
ina uzima wa milele unaotosha kuosha mauovu yetu.
Tunapomwamini kwa kumpa maisha yetu kama alivyotoa Maisha yake,
uhai katika damu yake unachukua nafasi yetu
na hutuweka huru, mbali na maovu yetu.
Kisha tunaweza kufurahia maisha pamoja naye, milele.