Inapakia video
Nakala
Swahili, Tanzania (Kiswahili)
Tunapopokea msamaha wa Mungu,
uhusiano wetu na Yesu unabadilikaje?
Kila mtu ameshindwa kuishi maisha safi.
Kwa hiyo tunajua kwamba tunamtegemea Mungu kwa kila jambo.
Anapotupatia msamaha na maisha mapya, Mungu anakuwa Mwokozi wetu.
Katika kutuwezesha kuishi maisha hayo mapya, yeye pia anakuwa Bwana wetu.
Bwana ni mtu anayeongoza na kuelekeza watumishi wake, ili wamfuate na kutii.
Anawalinda watumishi wake, na kuwapa kila kitu wanachohitaji ili kustawi, na kumtumikia.
Lakini yeye si Bwana wetu tu.
Pia anataka kuwa rafiki yetu wa karibu zaidi.
Kabla Yesu hajafa, aliwaita wafuasi wake marafiki.
Alipofufuka, kitu cha kwanza alichotaka kufanya, ilikua ni kushiriki mlo na marafiki zake.
Akawaonyesha jeraha mikononi mwake,
na ubavuni
Ili kuonyesha kwamba alikufa na kufufuka tena kwasababu aliwapenda, na alitaka kuwa nao milele.
Na kila siku yuko pamoja nasi,
Akisamehe, kuongoza, kuimarisha,
Na kutulinda na kila adui,
Ikiwa ni pamoja na uovu ulio ndani yetu.
Kama Mwokozi wetu, Bwana, na pia
Kama rafiki yetu.