Filamu Kamili
Magdalena
dakika 58FHD
Magdalena·44 sura
Magdalena
Magdalena, a film made especially for women, beautifully shares God's love and the gospel, engaging women at the heart level with the potential of changing their lives for eternity. A story of tenderness, freedom and purpose, it portrays Jesus' compassion for women and historical accounts of His interactions with them, as seen through the eyes of Mary Magdalene.
MaswaliMaswali Yanayohusiana
Uliza lakoNukuu za Biblia
ShirikiNakala
Swahili, Tanzania (Kiswahili)
Nardine Productions Ikishirikiyana na Inspirational Films, Inc. wanatuonyesha
Magdalena akifunguliwa kutoka katika aibu
Palestine 40 A.D.
Eee! huku huwezi kuniona mimi, ebu tuone kama uta nikamata! niko huku!
(Kicheko)
Huwezi kunikamata! niko huku! ebu nikamate!
Ahaa! Angalia!
Ni nzuri namna gani kazi atuonyeshayo Mungu kila siku jioni.
Inanikumbusha upendo wake mkubwa kwa ajili yangu.
Na kwako.
Mungu aliumba vyote hivi?
Nina shaka kama ananiona na mimi
Hani juwi hata kidogo.
Huenda Mwenyezi Mungu ange mpenda mtu mtakatifu
Lakini si mtu kama mimi
Rivka, laiti unge kuwa na mimi wakati huo wa myaka mitatu aliyo tufundisha.
Mwalimu, Yesu?
Safira.
Unge penda ku tuambia habari zake?
Ndiyo, tafathali tuambiye hadisi yake
Ndiyo, nta waambia,
Karibu.
Vyema
Lazima tuanziye mwanzo kabisa.
Ulipo kutana na Yesu?
Subiri, ili kufahamu hadisi ya Yesu, lazima tuanziye mwanzo kabisa.
Kama maandiko matakatifu yanavyo tu fundisha.
Hapo mwanzo, Mungu aliumba dunia na mimeya yote, wanyama, ndege, na viumbe vya baharini.
Tokana na udongo, alimfanya mtu wa kwanza.
Na aka mpulizia pumzi ya uhai katika puwa zake.
Mtu wa kwanza aliitwa Adamu.
Mungu aka sema, "Si vema mtu huyo awe peke yake. Nita mfanyia msaidizi wa kufanana naye."
Kisha Mungu aka towa ubavu wa Adamu, na ku tokana na huo, alimfanya mwanamke aitwaye Eva.
Adamu na Eva waliishi katika uwepo wa Mungu katika bustani nzuri aliyo waandaliya,
Iliyoitwa Edeni.
Mungu alitembea na ku zungumza pamoja nao bustanini.
Na ha kukuwa na mateso, manyanyaso, wala mauti.
Mungu ali mwambiya Adamu, "Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula
Walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile.
Kwa maana siku utakapo kula matunda ya mti huo, utakufa hakika."
Lakini siku moja Shetani alimjaribu Eva.
Mwanamke aka lichuma lile tunda akala.
Kisha aka mpa piya mumewe, aliyekuwa naye, naye akala.
Tendo la aibu la Adamu na Eva la kutotii, liliharibu utulivu wa bustanini.
Utulivu kati ya mwanamume na mwanamke,
Na mapatano kati ya Mungu na wao.
Mwanaume alilaaniwa na maisha ya taabu.
Na mwanamke aliongezewa uchungu wa kuzaa na ku tawaliwa na mumewe.
Lakini Mungu aliweka ahadi piya: kwamba siku moja uzao wa mwanamke,
Uta mponda nyoka kichwa.
Katika maandiko matakatifu, Mungu mwenye huruma
Ana zungumuza juu ya mpango wa kurejesha utulivu na heshima kwa uumbaji wake.
Alifunuwa sehemu ya mpango huo kwa nabii Abrahamu.
Abrahamu ali mwamini na kumheshimu Mungu.
Mungu ali muahidi kumbariki na ku wabariki watu wa mataifa yote kupitiya yeye.
Siku moja, Mungu alimpa mtihani Abrahamu.
Alimwambiya Abrahamu amchukuwe mtoto wake na amtowe sadaka.
Abrahamu alijuwa kwamba kupitiya mtoto huyu, Mungu aliahidi kumpa uzao mwingi,
Na kubariki mataifa yote, hata hivyo alimwamini Mungu na kumtii.
Mungu aliita
“Abrahamu!”
"Sasa najuwa kuwa unanitii, kwa kuwa huku nizuwiliya mwanao mwana wako wapekee."
Abrahamu akaangaliya kando akaona kondoo.
Aka mtowa awe sadaka ya kuteketeza badala ya mwanawe.
Mungu kumu patiya Abrahamu kondoo badala ya mwanawe ilikuwa ni ishara...
dokezo la mpango wake mkubwa.
Mpango huu unge haribu laana ya dhambi na mauti
Na kuwa rejesha wanaume na wanawake kwenye uhusiano wa karibu naye.
Kuli kuwa na msichana aliyeishi Nazareti ambaye alipozwa na mtu aliyeitwa Yosefu.
Jina lake aliitwa Mariya.
Bwana yu pamoja nawe na amekubariki sana!
Usi ogope, Mariya. Kwa maana ume pata neema kwa Mungu.
Uta beba mimba na kupata mtoto wa kiume
Na uta mwita jina lake Yesu.
Lakini mimi ni bikira.
Inawezekanaje?
Roho Mtakatifu atakujiliya, na nguvu za Mungu zitakufunika.
Mtoto utakaye mzaa atakuwa mkuu na ataitwa Mwana wa aliye juu.
Hata Elizabeti jamaa yako atapata mtoto katika uzee wake,
Na mwezi huu ni wa sita kwake yeye aliyeitwa tasa. Kwa kuwa hakuna lisilo wezekana kwa Bwana.
Mimi ni mtumishi wa Bwana.
Na iwe kwangu kama ulivyosema.
Ndiyo Mariya aka ondoka kwa haraka ku mtembeleya binamu yake Elizabeti.
Elizabeti!
Mariya!
Binamu Mariya!
Oh, ni kweli.
Lakini wewe ume barikiwa katika wanawake wote.
Naye uzao wa tumbo lako ame barikiwa.
Lime tokayaje kwangu jambo hili kubwa hivi
Hata mama wa Bwana wangu anitembeleye mimi?
Nilipo sikiya sauti ya kuamukiya kwako
Kitoto kikaruka kwa shangwe tumboni mwangu.
Moyo wangu wa mwadhimisha Bwana;
Na roho yangu imemfurahiya Mungu mwokozi wangu, kwa kuwa amenikumbuka mtumishi wake,
Tokeya sasa vizazi vyote vitaniita "mbarikiwa."
Yesu alizaliwa Bethlehemu mahali pa kuliya ngombe,
Kwa kuwa Mariya na Yosefu hawa kupata nafasi katika nyumba ya jamaa zao.
Kuli kuwepo malaika wengi waliotangaza kuzaliwa kwake.
Wakati ulipowadiya wa mtoto kutahiriwa, alipewa jina Yesu,
Ambalo lina maana "Mungu ana okowa."
Mariya na Yosefu walikwenda na mtoto hekaluni ili kumkabidhi mbele za Bwana.
Nilipo sikiya hadisi yake, nilijuwa Yesu ange kuwa zaidi ya nabii wa kawaida.
Malaika alikuwa na maana gani alipomwita Yesu "Mwana wa aliye juu?"
Hakika, huna maana kwamba Mungu alikuwa na uhusiano na mwamke?
Hapana! hapana, hapana.
Kumbuka Mariya ali kuwa bikira.
Mimba ya Yesu kweli ilikuwa ni muujiza kutoka kwa Roho wa Mungu.
Mungu anaweza kufanya lolote.
Je? huamini hili?
Kwa sababu ya mwanzo wake wakimuujiza
Yesu alizaliwa na mwanamke kama wewe na mimi.
Hata hivyo alikuwa zaidi yetu.
Tubuni dhambi zenu
Na mkabatizwe
Na Mungu ata wasamehe dhambi zenu.
Mungu, mwenyewe, alisema hili wakati Yohana Mbatizaji mwana wa Elizabeti,
Alipo kuwa anabatiza wanaume na wanawake katika mto Yorodani.
Nawabatiza kwa maji.
Lakini yuaja mtu mwenye nguvu kuliko mimi.
Ambaye mimi sistahili hata kulegeza kamba za viatu vyake.
Yeye ata wabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.
Ambaye ungo wake u mkononi mwake, atapepeta makapi na kukusanya ngano galani mwake.
Na Roho Mtakatifu akashuka juu ya Yesu kwa umbo la huwa.
Na sauti ika toka mbinguni na kusema
Wewe ndiwe Mwanagu Mpendwa. Nime pendezwa nawe.
Baada ya ubatizo, Yesu alisafiri kupitiya miji aki fundisha,
Na ujumbe wake uli kuwa wa kuthibitisha mamlaka yake.
Je? huyo si mtoto wa Mariya?
Ndiyo, ni yeye,
Nyamanza.
"Roho wa Bwana yu juu yangu,
Kwa maana ame nitiya mafutu kuwa hubiri maskini habari njema.
Ame nituma kuwatangaziya wafungwa kufunguliwa kwao na vipofu kupata kuona.
Kuwa acha huru walio nyanyaswa,
Na kutangaza wakati muafaka wa Bwana kuwa okowa watu wake."
Anena vema.
Leo maandiko haya yametimiya masikioni mwenu Kama mlivyo yasikia yakisemwa
Je? maandiko yametimiya?
Lakini Masihi tu ndiye ana weza kutimiza ahadi hiyo!
Tutafahamu vipi?
Maneno yake yaliwashangaza wengi,
Na miujiza yake ilisababisha wengi kuamini.
Ni yeye.
Anafanya tena.
Ni nani huyo?
Ni yule mwalimu toka Nazareti
Yesu.
Hujambo.
Sijambo.
Ondoka. Hutakiwi hapa.
Mwalimu mwache huyo. Usijinajisi bure hata kwa kumwangaliya.
Mariya.
Unataka nini kwetu Yesu Mnazareti?
Tuna kujuwa wewe ni nani Mtakatifu wa Mungu!
Kaa kimya!
roho chafu
Toka kwa mwanamke huyu.
Amekufa.
Amemuuwa!
Anataka kumgusa!
Hapana! mtu mtakatifu hawezi kufanya jambo kama lile!
Mariya
Bintu wa Abrahamu.
Ni mzima!
Yuko hai!
Ni muujiza!
Mtu huyu ni nani?
Hata pepo wana mtii!
Ni muujiza.
Ni muujiza.
Inawezekanaje?
Asante.
Nashukuru.
Nashukuru.
Asante.
Kuanziya wakati huo, nikawe mfuasi wake
Nilitaka kufanya kinacho mpendeza Mungu.
Kwa myaka mingi, niliishi katika aibu.
Lakini Yesu ali rejesha heshima yangu.
Nguvu yake iliwafukuza wale pepo wachafu.
Uuuu,
Safira!
Dina!
Ume sikiya Yesu akifundisha na umeona miujiza mingi aliyofanya.
Ndiyo.
Kwa hiyo unajuwa kwa nini niliacha kilakitu ili kumufwata yeye.
Na sikuwa peke yangu.
Tulikuwa wenye njaa, kimwili na kiroho, na tulihitaji mtu mmoja wa kutu onyesha njiya ya Mungu.
Baada ya myaka mingi ya mapambano na kukatishwa tamaa, wengi wetu tulikosa tumaini.
Bali Yesu alionekana kutowa tumaini popote alipokwenda.
Nani-nani huyo?
Kijana wa kiume. Mtoto pekee wa mjane.
Kijana, inuka!
Nabii mkuu ame tokeya katikati yetu!
Mungu amekuja kuokowa watu wake!
Mki wapenda wale tu wanao wapenda ninyi
Kwa nini mpokee baraka?
Hata wenye dhambi wapenda wa wapendao
Nanyi mkiwatendendeya mema wale wawatendeao mema
Kwa nini mpokeye baraka?
Hata wenye dhambi hufanya hivyo.
Ana wezaje kumgusa?
Ana wezaje kuzungumza naye?
Inakera?
La
Wapendeni adui zenu
Watendeeni mema.
Na mkikopesha msi tumaini kurudishiwa.
Ndipo mtapata thawabu kubwa
Nanyi mtakuwa wana wa aliye juu.
Kwa kuwa yeye ni mwema kwa wasiyo na shukurani na waovu.
Iweni na huruma.
Kama Baba yenu alivyo na huruma.
Yesu alifundisha kwamba Mungu humtendeya mema hata mwenye dhambi nyingi
si kama aduwi wa kumuangamiza,
Bali kama kondoo aliye poteya ambaye humutafuta ili kumwokowa na kumurejesha kundini mwake.
Hatu kujuwa maana ya hali ya kuwa thamini na kuwa penda watu
hata wale tulio wadharau makarini nyingi, chotara wenye desturi za kigeni walione kama hawafai,
Mpaka Yesu alipo chaguwa kusafiri kupitiya Samariya.
Ni mwanamke gani huyu ambaye watu wana mudharau?
Ni musamariya. Je? ubaya huu hautoshi?
Twende zetu. Tunataka kununuwa chakula, hatutaki kumuacha mwalimu akisubiri.
Je? utanipa maji ninywe?
Wewe ni muyahudi.
Mimi ni mwanamke musamariya.
Unawezaje kuniomba mimi maji?
Laiti unge lijuwa atowacho Mungu na ni nani akuambiaye nipe maji ninywe
Ungeli mwomba yeye
Naye angeli kupa maji yaletayo uzima.
Bwana
Huna kitu chakuchoteya maji na kisima ni kirefu.
Utayapata wapi hayo maji ya uzima?
Baba yetu Yakobo ndiye aliyetupa kisima hiki.
Yeye wanawe na mifugo yake walikunywa toka kisima hiki.
Je? wewe nimkubwa kuliko baba yetu Yakobo?
Kila anywaye maji haya ataona kiu tena.
Yeyote anywaye maji nitakayo mupa mimi Hataona kiu tena.
Maji nitakayo wapa yata kuwa chemichemi ndani yao
Yaki bubujika uzima wa milele.
Bwana
Unipe maji hayo!
Ili nisione kiu tena
Wala nisije hapa kuteka maji.
Nenda kamwite mumeo na urudi hapa.
Mimi...
Mimi sina mume.
Umesema vema unavyosema huna mume.
Kwa maana umekuwa na wanaume watano.
Na uliyenaye sasa siyo mume wako hasa.
Hapo umeniambiya kweli.
Bwana. Naona yakuwa u nabii,
Baba zetu wasamariya walimwabudu Mungu katika mlima huu.
Lakini nyinyi wayahudi husema Yerusalemu nimahali patupasapo kumwabudu Mungu.
Mwanamke, niamini, saa inakuja
Ambao hamuta mwabudu Baba katika mlima huu wala kule Yerusalemu.
Nyiye wasamariya mnaabudu msicho kijuwa.
Lakini saa inakuja Na ndiyo sasa
Wakati kwa uweza wa Roho wa Mungu watu watamwabudu Baba kama alivyo,
Wakifanya ibada halisi anayo taka.
Mungu ni Roho, ni kwa uweza wa Roho wake tu watu wataweza kumwabudu yeye kama alivyo.
Yule mwanamke
Ana fanya nini anapo zungumza naye?
Anamjuwa yeye ni nani?
Najuwa
Masihi atakuja.
Na atakapo kuja, atatwambiya kila kitu.
Mimi ndiye.
Njooni mumuone yule mtu aliyeniambiya mambo yote niliyowahi kuyatenda. Njooni.
Anaweza kuwa ndiye Masihi?
Masihi?
Masihi?
Aliyeahidiwa (kuja)? (hapana) haiwezekani.
Njooni mumuone. Njooni.
Mwalimu, kula kitu!
Mimi nina chakula msicho kijuwa.
Je? kuna mtu amemuleteya chakula?
Chakula changu
Ni kuyatenda mapenzi yake aliye nituma
Na kuyimaliza kazi yake aliyonipa.
Mazao yame kwisha komaa
Tayari kwa mavuno!
Tazama wangapi wanakuja!
Na habari njema kwa wasamariya, piya?
Watu toka mjini walimujiya Yesu na kumusihi akae kwao na kuwafundisha.
Tulikaa kwa siku mbili, na wasamariya wengi wakamwamini yeye.
Yupi kwenu akijisumbukiya, anaweza kujiongezeya maisha yake?
Ikiwa hamuwezi kujitendeya neno hilo ndogo kwa nini kujisumbukiya kwa yale mengine?
Tafakarini mauwa, jinsi ya meavyo,
Hayatendi kazi wala hayasokoti
Hata Solomoni katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama hayo.
Ikiwa Mungu
Huvika hivi majani ya kondeni kesho hutupwa motoni
Je? hata wavika ninyi zaidi?
Enyi wa imani haba.
Tuongezeye imani zaidi.
Kama mungekuwa na imani kiasi cha punde la haradali, munge uambiya mti huu wa mkuyu
Ngoka ukajipandikize baharini, nao unge watii.
Makwazo hayana budi kuja.
Lakini ole wake ambaye yaja kwasababu yake.
Inge mfaa zaidi mtu huyo jiwe lakusagiya lifungwe shingoni mwake
Akatupwe baharini, kuliko kumkosesha mmoja wapo wa wadogo hawa.
Ufalme wa Mungu umefanana je?
Uko namna hii:
Mtu anaye twaa punje la haradali na kulipanda shambani mwake.
Ikameya ikawa mti mkubwa ndege wa angani wakakaa katika matawi yake.
Sina hakika anazungumziya nini.
Kwa nini unakula na kunywa pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi?
Wenye dhambi?
Wenye afya hawahitaji dactari, isipokuwa wale ambao ni wagonjwa.
Sikuja kuwaita wenye haki bali wenye dhambi wapate kutubu.
Nikiyagusa mavazi yake tu.
Nitapata uponyaji.
Ninani aliyenigusa?
Kuna mtu aliyenigusa.
Maana naona nguvu zimenitoka.
Ni mimi niliyekugusa.
Nimeteseka myaka kumi na mbili nikitoka damu.
Nimetumiya mali zangu zote kuwapa waganga bila kupona.
Lakini nilipogusa vazi lako tu
Nika pona.
Binti
Imani yako imekuponya.
Nenda kwa amani.
Asante.
Alimwita yeye "binti?"
Ndiyo, mtu ambaye alikuwa najisi kwa myaka kumi na mbili kutokana na sheriya zetu.
Aliona aibu yake na kumurudishiya heshima yake.
Sijuwi nikipi kinacho leta uponyaji mkubwa hivi.
Nguvu ya Yesu
Au huruma yake.
Msiogope, enyi kundi ndogo, kwakuwa Baba yenu anaona vema kuwapa ule ufalme.
Viuzeni vyote mlionavyo muwape maskini.
Jifanyiyeni mifuko isiyochakaa jiwekeyeni hakiba isiyopunguwa mbinguni,
Mahali ambapo hazitapunguwa
Mahali asipoweza mwizi kuzikaribiya.
Wala nondo kuharibu
Kwa kuwa niya yako ilipo ndipo utakapokuwapo na mayo wako,
Mwanamke
Umepona katika ugonjwa wako.
Angaliya! angaliya, amepona! nimiujiza! angaliya, angaliya, amepona! njooni, muone!
Muujiza mwingine!
Si-si- si-sifa
Kwa Bwana!
Myaka kumi na nane!
Mungu akulinde, Mwalimu!
Kuna siku sita za kufanya kazi.
Njooni kati ya siku hizo ili mponywe, lakini siyo siku ya sabato.
Enyi wanafki!
Yeyote kati yenu amfunguwe punda au ngombe wake zizini siku ya sabato?
Aende naye kumnywesha maji,
Nahapa yuko binti wa Abrahamu ambaye Shetani alimfunga myaka kumi na nane.
Je? haimpasi kufunguliwa siku ya sabato?
Mwenye dhambi!
Mzinzi!
Mzinzi!
Kahaba!
Mzinzi!
kahaba!
Mwalimu
Mwanamke huyu tumemshika katika tendo la kufanya uzinzi.
Katika sheriya zetu, Mose alituamuru
Kwamba mwanamke kama huyu apigwe mawe hadi kufa.
Ndiyo, apigwe!
Kahaba! apigwe!
Ndiyo, apigwe mawe! apigwe mawe!
Kahaba! apigwe mawe!
Apigwe mawe!
Wewe wasema je?
Mwalimu, sisi tuna ushahidi wa watu wawili.
Tufanye nini na mwanamke huyu?
Yeyote kati yenu ambaye hajawahi kutenda dhambi, naawe wa kwanza kumtupiya jiwe.
Mwanamke
Wako wapi wale?
Je? kuna aliyebakiya kukuhukumu?
Hakuna, Bwana.
Wala mimi sikuhukumu piya.
Nenda sasa, na uache maisha yako ya dhambi.
Tafathali niinuwe.
Haya panda begani mwangu. Je? unaweza kuona sasa?
Namuona Yesu.
Anaasi sheriya.
Mpanzi alikwenda kupanda mbegu.
kwa kuvunja sabato
zingine zilianguka karibu na njiani zikakanyagwa.
Akishiriyana na wenye dhambi.
Tukimwacha hivi hivi
Watu wote watamwamini
Watawala wa kiroma watachukuwa hatuwa ya kuharibu hekalu letu.
Walishindwa kumnasa Yesu au kupunguza wafuasi wake,
Lakini waliazimiya ku simamisha madai yake kuwa yeye ni Masihi.
Nawalimpata mtu mmoja aliyetayari kumsaliti.
Maranyingi Yesu aliwapeleka wafuasi wake mlima wa mizeetuni ili kuomba.
Usiku ule alisumbuka sana rohoni.
Mbona mmelala?
Amkeni
Muombe msije mukaingiya majaribuni.
Yuda
Ni kwa busu unamsaliti mwana wa mtu?
Bwana, Je? tuwapige kwa upanga?
Mkamateni.
Yatosha!
Je? ninyi mmekuja na mapanga na marungu kunikamata kana kwamba ni myanganyi?
Nili kuwa nanyi siku zote hekaluni na hamu kunitiya nguvuni.
Lakini huu ni wakati wenu wa kutenda
Wakati wa nguvu za giza kutawala.
Mkamateni!
Rafiki yake amemsaliti?
Mmoja wa wafuasi wake?
Mtu ambaye tulimfahamu kweli na kumwamini.
Mlindeni vema.
Usiku ule, walinzi walimdhihaki na kumpiga.
Nani amekupiga?
Tabiri!
Nani atakupiga tena?
Acha!
Acha, nasema!
Aletwe mbele ya baraza.
Tuambiye
Je? wewe ndiye Masihi?
Hata nikiwaambiya
Hamtanisadiki.
Nahata kama nikiwauliza swali hamta nijibu.
Lakini tangu sasa Mwana wa mtu atakuwa ameketi upande wa kuliya wa Mungu mwenyezi.
Kwa hiyo wewe,
Ni Mwana wa Mungu?
Wewe wasema mimi ndiye.
Anena kufuru!
Je? kunahaja ya ushahidi mwingine?
Nani amempa mamlaka kunena haya?
Sasa mmesikiya kukufuru kwake!
Hatiya!
Sisi wenyewe tumesikiya kile alichosema.
Anahatiya na anastahili kufa!
Tutampeleka kwa Pilato.
Ndiyo, ndiyo, mwondowe!
Kwahiyo wakampeleka kwa gavana wa kiroma, Pontiyo Pilato.
Kiongozi mkatili, aliyeitwa Pilato alihusika kusulubiwa kwa maelfu ya watu.
Munataka nini hapa, asubuhi yote hii?
Tumemkamata mtu huyu akipotosha watu wetu.
Alileta gasiya katika soko la hekalu.
Tumemuona ana hatiya, akiambiya watu wasilipe kodi kwa Kaisari, akidai yeye ni Masihi,
Mfalme.
Mfalme?
Je? wewe ni mfalme wa wayahudi?
Wewe wasema.
Hatuna mfalme mwingine bali Kaisari.
Tuna sheriya, na kwa sheriya yetu anastahili kufa, kwa sababu yeye alidai ni Mwana wa Mungu.
Mtu huyu
Haja fanya jambo linalostahili kifo.
Kwa hiyo nitampeleka achapwe
Nanita mwachiliya.
Kama ukimwachiliya, wewe si rafiki wa Kaisari!
Msulubishe!
Ndiyo, msulubishe!
Wewe, wewe, mchape.
Kila mtu anayejidai kuwa mfalme anaasi kinyume cha Kaisari.
Unangojeya nini, Pilato?
Mwondowe huyo! muuwe! msulubishe!
Hajafanya lolote baya.
Msulubisheni!
Msulubisheni! msulubisheni!
Nyuma! Rudi nyuma!
Nyuma!
Rudi nyuma!
Ondoka njiana!
Kaa mbali naye!
Rudi nyuma! Rudi nyuma!
Ondoka!
Towa nafasi!
Ondoka!
Wewe, Pisha njaya!
Sogeya na kwambiya!
Amuka!
Wewe, beba.
Haya, tembeya!
Nyuma!
Nyuma!
Inuwa msalaba!
Wasamehe, Baba
Kwakuwa hawajuwi watendalo.
Je?
Wewe
ni Masihi?
Jiokowe
wenyewe
Na sisi.
Je? hu mwogopi Mungu?
Tumepata hukumu moja
Kama yeye
Lakini Hajafanya kosa lolote.
Nikumbuke, Yesu
Uta ka--po ingiya katika ufalme wako.
Nakuahidi
Leo hii tutakuwa paradizo pamoja.
Nami.
Ilipo fika adhuhuri, anga likawa giza kwa saa tatu.
Baba
Mikononi mwako
Nayiweka
roho yangu
Utukufu kwa Mungu hakika mtu huyu alikuwa mwenye haki.
Ali kuwepo mtu moja wa baraza la kidini
alikuwa mwenye haki ambaye hakushiriki katikakumu hukumu Yesu.
Jina lake iliitwa Yosefu wa Arimatheya.
Alipata kibali kutoka kwa Pontiyo Pilato
Kuuweka mwili wa Yesu katika kaburi la karibu kwakuwa sabato ilianza panapo machoo ya juwa.
Samahani.
Tunaufwata mwili wa Bwana wetu.
Karibuni nyote.
Lakini njooni
Sabato inakaribiya.
Kwa nini waliamuwa kumuuwa?
Ikiwa alitoka kwa Mungu, kwa nini aliruhusu wamuuwe?
Niliulizwa maswali hayo yote.
Yesu alikuwa na uwezo juu ya pepo wabaya.
Hata na wafu walimsikiliza
Je? asingezuwiya hili?
Nilimufwata kwa myaka mitatu nikitegemeya kuwa ndiye Masihi aliahidiwa
Lakini sasa ameondoka.
Naninge kwenda wapi?
Hadisi hii niya kusikitisha.
Lakini, inamwisho wenye utukufu.
Asubuyi ya juma pili, siku ya tatu baada ya Yesu kusulubiwa,
Tulikwenda kaburini tukichukuwa manukato tuliyo andaa kwa kuupaka mafuta mwili wake.
Jiwe limeviringishwa mbali.
Petro... Yakobo... Yohana... sikilizeni.
Jiwe limeviringishwa mbali!
Tuliingiya, lakini mwili wa Bwana wetu haukuwepo.
Wamemwondowa Bwana kutoka kaburini, na hatujuwi wapi wamempeleka!
Nini? mwili wa Bwana wetu, haupo?
Nenda ukajioneye mwenye.
Baada ya kulichunguza kaburi, Petro alirudi kwa wanafunzi wengine.
Lakini mimi nilibaki inje ya kaburi, nikiwaza, na kuliya.
Lazima askari wamemchukuwa
Au mafarisayo.
Waliviuwa vyote tuvyo tumainiya.
Angalau wange tuachiya mwili wake tu.
Mwanamke, kwa nini unaliya?
Wame mchukuwa Bwana wangu
Na sijuwi wamempeleka wapi.
Mwanamke, kwa nini unaliya? Ni nani ambaye unamtafuta?
Bwana
Kama ulimchukuwa wewe
Niambiye wape ulimpeleka, ili niende nikamchukuwe.
Mariya.
Mwalimu!
Usinishike kwa sababu sijapaa kwenda kwa Baba.
Uko hayi, Bwana!
Nenda, kawape habari hii ndugu zangu.
Hujatusahau sisi, Mungu hajatuacha.
Waambiye.
Nime mwona Bwana!
Nime mwona Masihi!
Amefufuka?
Ndiyo.
Ki vipi?
Mauti haikuweza kumshika.
Sasa kwa nini ilimpasa kufa? Ili kushinda mauti.
Ah, mimi sikuelewa siku ile,
Lakini Yesu alitutokeya mara nyingi baada ya hapo
Na akatufundisha.
Mamiya ya myaka kabla ya Yesu kuja,
Manabii walitabiri katika maandiko kwamba Masihi aliyeahidiwa angeteseka.
Isaya ameandika, "Alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu;
Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, na kwa kupigwa kwake sisi tumepona."
Nabii Mose alisema, "Amelaaniwa na Mungu yeye aliyetundikwa juu ya mti."
Yesu alipo kufa msalabani, ali chukuwa juu yake mwenyewe laana - laana yangu - ya dhambi, na mauti.
Kujitowa kuwa sadaka na kufufuka kwake vimetuweka huru na kifungo cha uovu,
Ametuokowa toka nguvu za giza, na kutukombowa tokana hofu ya maisha na aibu.
Baraka hii ndiyo Mungu alimuahidi Baba yetu Abrahamu,
Aliposema kuwa watu wote wa duniya watabarikiwa kupitiya yeye.
Watu wote?
Hata wanawake?
Yesu aliniita mimi "binti wa Abrahamu."
Wewe ni binti unayependwa
binti ambaye anatakakubariki
Kama mwanamke yule aliyemponya kutoka kuvuja damu myaka kumi na mbili...
Au kama mimi.
Hakuna kati yetu anayestahili kuishi katika hofu na aibu.
Hatupaswi tujisikiye tena hatuonwi wala hatusikiwi.
Yesu alijineneya mwenye:
"Roho wa Bwana yu juu yangu
Kwa maana ametiya mafuta kuwahubiri maskini habari njema.
Amenituma kuwa tangaziya wafungwa kufunguliwa kwao na vipofu kupata kuona
Kuwaacha huru waliyonyanyaswa
Na kutangaza wakati muafaka wa Bwana wa kuwaokowa watu wake."
Yesu aliwagusa watu,
hata wanawake waliyoshambuliwa na magonjwa ingawa walihesabiwa kuwa najisi
Na aliwaponya.
Alifundisha watoto, wanaume na wanawake, tajiri na maskini,
wenye haki na wenye dhambi, kuwarejesheya utu wao
Na kudhihirisha huruma zake nyingi.
Aliwaponya watu
Akiwatowa pepo, akiwaweka huru wanaume, wanawake, na watoto kutoka vifungo vya Shetani.
Hii inadhihirisha mamlaka yake juu ya pepo wabaya na kila roho.
Yesu aliwarudishiya uhai wana na mabinti waliyo kufa
Akionyesha anauwezo
Hata juu ya mauti.
Na ingawa Shetani na roho chafu
waliamini walifanikiwa kupata ushindi wakati walipo mtundika Yesu msalabani,
Yesu alifufuka kutoka ufuni, akishinda juu ya nguvu zote za uovu na mauti.
Kwahiyo alikuwa Masihi?
Ni Masihi tu aliyeahidiwa aliyetumwa na Mwenyezi Mungu angeweza kufanya miujiza ambayo Yesu alifanya.
Ni mtu mwenye huruma tu, na uwezo,
na kuaminika kama Yesu anastahili kuaminiwa na kuabudiwa nasi.
Mungu alipoumba ulimwengu,
Alimfanya mwanaume na mwanamke waishi katika uwepo wake na kupata furaha yake.
Huo ndio ulikuwa mpango wake.
Lakini hatukumwamini, na hatukutii amri yake.
Tendo hili la aibu lilitutenganisha na Mungu,
na kuharibu uhusiyano wa karibu kati ya mwanamke na mwanaume.
Nasisi, piya, tumeendeleya katika uasi huo.
Maandiko yana sema, " Hakuna mtu asiyetenda dhambi."
Matokeo ya dhambi hii ni mauti na kutengana na Mungu.
Lakini Mungu hakuridhika kuona sisi tunabaki tumetengwa naye na upendo wake,
tukiishi kwa aibu na hofu.
Hivyo, kama alivyotowa kondoo kufa badala ya mtoto wa Abrahamu, Mungu alimtuma Yesu kufa badala yetu.
Maisha ya Yesu, kufa, na kufufuka kwake kulirejesha uhusiyano kati ya Mungu
Na wale wanaomgeukiya na kumufwata.
Na uhusiyano huu wa karibu na Mungu mwenyezi haukomi, hata tukifa.
Muhalifu pale msalabani, alipokaribiya kufa, alimwamini Yesu...
Na Yesu alimuahidi, " Leo hii utakuwa nami paradizo."
Wale wote wanao weka tumaini lao kwa Yesu
wataepuka adhabu ya milele na kuishi na Mungu milele.
Inakuwaje?
Kwakumufwata yeye kwa imani.
Lakini atanikubalije mimi?
Alimkubali Mariya na mimi.
Nitajuwaje?
Mwamini.
Mwombe.
Zungumza naye.
"Mungu, Baba wa mbinguni
U mtakatifu na wa haki.
Asante kwa kunipenda.
Nime kutenda dhambi.
Asante kwa kumtuma Masihi aliyeahidiwa, Yesu
Ilikuharibu laana ya aibu na hatiya.
Nashukuru kuwa alikufa kwaajili yangu.
Ninataka kumufwata mwokozi wangu aliye hayi.
Nakushukuru kwa kunisamehe na kuni kubali mimi.
Amina.
Amina.
Amina.
Asante.
Asante.
Yesu alisema, "Kondoo wangu
Waisikiya sauti yangu.
Nami nawajuwa
nao wanifwata."
Anakujuwa, Rivka
na anakupenda.
Huu ni mwanzo wa uhusiyano wa milele
Ambao unakuwa
Tunavyo zidi kumujuwa zaidi
na kumutumaini zaidi.
Tunakuwa tunapolitii neno lake
na kumwomba kwa imani
Nakuwa pamoja na wamufwatao.
Na kuwaambiya wengine kuhusu yeye, na kuyazingatiya tuliyoambiwa na Yesu:
Bwana awabariki na kuwa linda.
Mamlaka yote mbingu na duniani nimepewa mimi.
Basi nendeni, mkayafanye mataifa yote kuwa wanafunzi,
Mtabatiza kwa jina la Baba, na la Mwana, na Roho Mtakatifu,
na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi.
Natazama mimi nipamoja nanyi sikuzote, hata mwisho wa ukamilifu wa ulimwengu.