Inapakia video
Nakala
Swahili, Tanzania (Kiswahili)
Nani kati yenu atanifwata?
Nita kufwata Bwana
Lakini kwanza, niruhusu niage wa nyumbani kwangu.
Mtu aliyetiya mkono wake kwa kulima kisha akaangaliya nyuma hafai kwa ufalme wa Mungu.
Mtu yeyote akitaka kunifwata, na ajikane mwenyewe Ajitwike msalaba wake kilasiku, na anifwate.
Kwakuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake atayiangamiza
Na mtu atakaye angamiza nafsi yake kwa ajili yangu atayiponya.
Itamfaa nini mtu kuupata ulimwengu wote kama ataipoteza nafsi yake mwenyewe?
Ikiwa mtu atanioneya haya mimi na maneno yangu
Mwana wa mtu atamwoneya haya atakapo kuja katika utukufu wake
Na utukufu wa Baba na wamalaika watakatifu.
Nawaambiya kweli
Wapo watu hapa ambao hawataonja mauti kabisa hata wauone kwanza ufalme wa Mungu.